Mambo Matatu Muhimu ya Kuzingatia Ukiwa Unajifunza Lugha Yoyote Ngeni.






Karibu msomaji wa mtandao wa LEARN ENGLISH LANGUAGE,karibu katika somo la leo ambapo tutajifunza mambo muhimu ya kuzingatia ukiwa unajifunza lugha yoyote ngeni.Hivyo sisi tunajifunza lugha ya kiingereza hatuna budi kujifunza na kuzingatia mambo haya.Unapojifunza lugha ya kiingereza unatakiwa kuangalia kila neno katika njia tatu:


  1. Maana ya neno :Meaning of the word.
Elewa maana halisi ya neno lolote katika lugha ya kiingereza,hii itasaidia kuelewa maana ya maneno mengine kwa wakati huohuo.

Understanding the meaning of words in English can help you to understand the meaning of other words at the same time.

Example : Mfano
Boy - mvulana
Ukisha jua boy ni mvulana kwa kiingereza lazima katika akili yako utajiuliza msichana anaitwaje kwa kiingereza,lazima utatafuta kujua msichana anaitwaje,tayari utakuwa umejifunza neno jipya.


2. Aina za maneno :Parts of speech

Kuna aina nane za maneno zinazotumika katika lugha ya kiingereza,kama unataka kujua kuongea,kuandika na kusoma vizuri lazima ujue aina za maneno,tambua kwamba kila aina ina sheria zake katika maandishi,matamshi na matumizi.Ni lazima ujifunze kutambua kila neno liko kwenye kundi lipi.Hizi ndio aina za maneno:

  • Noun   - Jina
  • Verb - Kitenzi
  • Pronoun - Kiwakilishi
  • Adjective - Kivumishi
  • Articles - Viambatanishi
  • Adverb - Vielezi
  • Preposition  - Viunganishi 
  • Conjuction - Vihusishi


Soma:Zijue Aina za maneno(Parts of Speech)

   3.  Matumizi ya neno :Uses of  word
Kila neno lina matumizi yake katika kukamilisha maana ya sentensi,ukitambua matumizi ya kila neno ni rahisi kwako kutambua viambatanishi ili kukamilisha sentensi.
Mfano chunguza sentensi zifuatazo matumizi ya neno "What"

  • what  is on the table? - Kuna nini juu ya meza?
  • What is she doing? - Yeye anafanya nini?
  • What are you talking about?- Wewe unaongea kuhusu nini?
Hapa utagundua neno "what" lina matumizi kofauti katikakila sentensi.

Msomaji wa LEARN ENGLISH LANGUAGE hayo ndio mambo matatu muhimu ya kuzingatia ukiwa unajifunza lugha ya kiingereza ambayo ni lugha ya kimataifa.Jifunze lugha ya kimataifa kwa kujiunga na mtandao huu ili uweze kupkra mafunzo uweze kuendelea kujifunza kupia email yako.Bonyeza hapa hapa kujiunga na mtandao wetu.karibu tujifunze pamoja.






0 comments:

Post a Comment