Ni siku nyingine tena msomaji wa LEARN ENGLISH LANGUAGE napenda kukukaribisha katika somo la leo ambapo tutajifunza maana ya viwakilishi (pronouns) na viwakilishi vya nafsi (Personal Pronoun) vinavyotumika katika lugha ya kiingereza.Karibu tujifunze pamoja.
PRONOUN : KIWAKILISHI
Pronoun ni neno linalosimama badala ya jina/nomino.
Hii inamaanisha neno hilo linawakilisha jina,viwakilishi vinaweza kusimama badala ya jina la mtu,sehemu,vitu hata wazo.Matumizi ya viwakilishi hayaluhusu majina kuandikwa tena katika sentensi kwa sababu tayari kiwakilishi kimesha wakilisha jina.
Pronoun is a word that stand instead of noun.
This means that pronoun represents nouns.A pronoun can represent a name of person,place,things or an idea.The use of pronoun does not allow to rename the noun which is represented or replaced in the sentence.
PERSONAL PRONOUNS : VIWAKILISHI VYA NAFSI
Personal Pronouns ni viwakilishi vinavyowakilisha nafsi za watu.Viwakilishi hivi vipo katoka mifumo tofauti kulingana na uwepo wa watu,idadi na jinsia.
Kuna nafsi ya kwanza umoja na wingi ( "I : mimi "and "WE : sisi")
kuna nafsi ya pili umoja na wingi ("you : wewe")
kuna nafsi ya tatu umoja na wingi ("she,he,it" and "They")
Katika lugha ya kiingereza person pronouns zimegawanyika katika makundi saba ambayo ni I,WE,YOU,SHE,HE,IT and THEY.
1. I : MIMI
Hiki ni kiwakilishi cha nafsi ya kwanza umoja cha jina binafsi.Kiwakilishi hiki hutumika pale mtu unapojizungumzia wewe mwenywe.Hii ndio sababu inaitwa nafsi ya kwanza umoja.
Mfano /Example
Mimi huwa naenda mjini kila siku
I go to town everyday
2. WE : SISI
Kiwakilishi hiki ni cha nafsi ya kwanza wingi.Hutumika pale mtu anapozungumzia jambo na yeye anakuwa mmoja wa wahusika wote.Husimamia majina ya watu wengi,wanaweza kuwa wanawake au wnaume au wote kwa pamoja.
Mfano /Example
Mimi,John na Neema tunaenda kanisani
I,John and Neema are going to the church
We are going to the church.
Sisi tunaenda kanisani.
3. YOU :WEWE /NINYI
Kiwakilishi hiki husimama badala ya jina moja au mengi,huwakilisha nafsi ya pili umoja na wingi,
na hutumika kwa jinsia zote.Pia hutumika pale mtu unapomzungumzia mtu mwingine ndio maana
inaitwa nafsi ya pili.
Mfano /Example
Wewe lazima ufanye kazi kwa bidii ili ufanikiwe
You must work hard in order to succeed
4. THEY : WALE /WAO.
Kiwakilishi hiki husimamia majina ya watu wengi kwa pamoja wanaweza kuwa wanaume au
wanawake au wote kwa pamoja.
Mfano / Example
Jenny na John wanasoma vitabu
Jenny na John are reading books
They are reading books
5. HE : YEYE
Kiwakilishi hiki husimamia jina la wanaume tu.Badala ya kutumia jina la mwanaume yule kiwakilishi
chake hutumika kiwakiliska jina.
Mfano / Example
John ni baba yangu , John huwa ni daktari
John is my father,John is a doctor.
He is my father,he is a doctor
6. SHE: YEYE
Hiki ni kiwakilishi cha nafsi ya tatu umoja,huwakilisha jina la mwanamke tu.Ni nafsi ya tatu umoja
kwa sababu tunamzungmzia mtu yule na yuko peke yake na jinsia ya kike.
Mfano / Example
Mariana ni mwalimu mzuri sana wa saikorojia.
Mariana is a good teacher of psychology.
She is a good teacher of psychology.
7. IT : Ni kiwakilishi kinasimamia majina ya vitu vyote isipokuwa majina ya watu.Lakini pia
mtoto mchanga hutumia kiwakilishi hiki.
Mfano /Example
Ile ni gari yangu,ninaimiliki mimi.
That is my car,it is belongs to me.
Gari imeibiwa
A car has stolen
It has stolen
Msomaji wa mtandao wa LEARN ENGLISH LANGUAGE tutaendelea kujifanza viwakilishi vingine vinavyotumika katika lugha ya kiingereza.Endelea kuwa nasi na kama hujajiunga na mtandao huu jiunge sasa ili kuweza kujifunza zaidi lugha ya kimataifa.
Your Tutor
Jenicia John
http://tlearningenglish.blogspot.com
It's very nice, thank you a lot tutor J for the lesson.
ReplyDeleteThe use of a simple language, makes it easier to understand. Keep it up.
This comment has been removed by the author.
ReplyDeleteThank you very much
ReplyDelete