TODAY'S LESSON PLAN
* Maana ya Vibainishi - Meaning of Articles
* Aina za Vibainishi -Kind of Articles
* Matumizi ya Vibainishi - Uses of Article
* Misamiati ya leo - Today's Vocabolaries
* Zoezi - Exercise
* Hitimisho - Conclusion.
Habari za leo msomaji wetu natumaini unaafya njema kabisa ndio maana unaendelea kuweka jitihada kubwa katika kuendelea kujifunza lugha ya kiingereza pamoja na sisi.Tuko hapa kuhakikisha unaelewa na kuweza kutumia lugha hii kwa ufasaha na ufanisi zaidi. Karibu ndugu msomaji katika somo la leo ambapo tutajifunza vibainiahi vinavyotumika katika lugha ya kiingereza.Katika lugha ya kiingereza hasa majina ya vitu hutanguliwa na neno lingine kabla halijatamkwa,neno hilo huitwa kibainishi (Article)
VIBAINISHI - ARTICLES
Vibainishi ni maneno yanayowekwa kabla ya majina ili kuyabainisha.Vibainishi hinyo ni "A","AN" na "THE".
Articles are words placed before nouns to identify them.Articles include "A", "AN" and "THE".
Mfano:
A tree
AN Orange
THE Bible
kutoka kwenye hiyo mifano mitatu hapo juu tutapata aina za vibainishi
AINA ZA VIBAINISHI - KINDS OF ARTICLES.
Kuna aina mbili za vibainishi - There are two kinds of articles
- Indefinite Articles - Vibainishi visivyo dhihirishi
- Definite Article - kibainishi dhihilishi
1. INDEFINITE ARTICLES:"A","AN" - VIBAINISHI VISIVYO DHIHIRISHI "A","AN"
Hivi ni vibainishi vinavyo simama mwanzoni mwa majina yote yenye maana ya kitu kimija chochote.Hii inamaanisha kwamba vibainishi hivi haviwezi kusimamia majina yaliyo katika hali ya wingi.
Vinaitwa vibainishi visivyo dhihirishi kwa sababu vinasimamia jina la kitu chochote kile bila ya kueleza kwa undani kuhusiana na kitu kile.Angalia sentensi inayofuata:
I saw John carring a book - Nilimuona John amebeba kitabu.
Katika sentensi hii John alionekana amebeba kitabu lakini haijulikani kile ni kitabu gani?,cha nini? .Ndio sababu kibainishi "a" kinetumika hapo haijulikani John alikuwa amebeba kitabu gani hakuna anaeweza kudhihirisha ila kile kilikuwa ni kitabu tu.
NOTE:Vibainishi hivi hutofautiana matumizi kutokana na matamshi ya majina vinayoyasinamia,chunguza sentensi zifuatazo:
- "A" Kibainishi hiki husimamia majina yanayoanza na konsonanti tu,pia huweza kusimamia majina yanayoanza na irabu inapotamkwa kama konsonanti.
A table - meza
A house - nyumba
A car - gari
A Uniform - sare
A Universal - ulimwengu
Katika hiyo mifano hapo juu mfano wa kwannza mpaka wa tatu,a table,a house,a car,haya yote ni majina yanayoanza na konsonanti na yote yako katika hali ya umoja ndio maana article "a" imetumika.kuvibainisha na matamshi yake yanaanza na konsonant.Na katika mfano wa nne na tano,a Uniform,a Universal,haya yote ni majina yanayoanza na irabu lakini katika matamshi inatoka sauti ya konsonanti.
a table - e tebo
a house - e haus
a car - e kaa
a Uniform - e juniform
a Universal - e juniverso
2. "AN" Kibainishi hiki husimama katika majina yanayoanza na irabu tu,na majina yanayuanza na konsonati zinazotamkwa kama irabu..
Mfano:
An hour - en awa
An orange - en orenji
An honest citizen - en onest citizen
Kila siku tutajifunza misamiati 5,matamshi na maana yake.
Msamiati - Matamshi(pronounciation) - Maana(meaning)
- Abandon - - - telekeza
- Abandoned - - - telekezwa
- Abandoning - - - kuacha
- Abesemeny - abeziment - fedheha
- Abash - - aibisha
EXERCISE - ZOEZI
1. Andika maneno 10 ya kiingereza yalnayotanguliwa na kibainishi "a"
2. orodhesha maneno 10 yanayotanguliwa na kibainishi "an"
Conclusion - Hitimisho
Kujua vema vibainishi visivyo dhihilishi soma vitabu vya kiingereza na chunguza kwa makini sehemu ambayo vibainishi hivyo vimetumika .Utagundua mambo mengi sana kwa njia hii ya kujisomea mwenyewe.Kama unaswali lolote usisite kuuliza Mwalimu niko kwa ajili yako ni furaha yangu kuona unajua lugha ya kimataifa.
Karibu tujifunze pamoja.
Your Tutor
JENICIA JOHN
http://tlearningenglish.blogspot.com
Lucky Club Casino Site - Login and Register - LuckyClub
ReplyDeleteLucky Club Casino Review · Experience our site at Lucky Club Casino. Join us today and play with the best bonuses and promotions luckyclub.live for our players.