Personal Information

Taarifa Binafsi

Katika somo hili tutajifunza jinsi ya kuuliza na kutoa taarifa rahisi kuhusu mtu kwa Kiingereza.

1. Useful Questions – Maswali Muhimu

What is your name?
Jina lako nani?

How old are you?
Una umri gani?

Where are you from?
Unatoka wapi?

Where do you live?
Unaishi wapi?

What do you do?
Unafanya kazi gani?

2. Useful Answers – Majibu Muhimu

My name is Amina.
Jina langu ni Amina.

I am 25 years old.
Nina miaka 25.

I am from Tanzania.
Ninatoka Tanzania.

I live in Meatu.
Ninaishi Meatu.

I am a teacher.
Mimi ni mwalimu.

3. Short Dialogue – Mazungumzo Mafupi

John: What is your name?
Amina: My name is Amina.

John: How old are you?
Amina: I am 25 years old.

John: Where are you from?
Amina: I am from Tanzania.

John: What do you do?
Amina: I am a teacher.

4. Practice – Zoezi

Jibu maswali yafuatayo kwa Kiingereza:

  1. What is your name?
  2. How old are you?
  3. Where are you from?
  4. Where do you live?
  5. What do you do?

⭐ Challenge

Jaribu kujitambulisha kwa kutumia sentensi 5 za Kiingereza ulizojifunza katika somo hili.

Example:

My name is Asha.
I am 25 years old.
I am from Tanzania.
I live in Meatu.
I am a teacher.

📢 Endelea Kujifunza

Endelea kufuatilia Jenicia English Academy kwa masomo zaidi ya Kiingereza kutoka Beginner hadi hatua za juu.

Learn English. Build Confidence. Change Your Future. 🌱📚

Join us : https://chat.whatsapp.com/HGqqKlRReds00q1dKt9M2c?s=cl&p=a&ilr=0

Topic: Greetings – Salamu

Lengo la somo: Baada ya somo hili, mwanafunzi ataweza:
Kusalimia kwa Kiingereza.
Kuuliza mtu hali yake.
Kujibu anapoulizwa hali.
Kuaga kwa Kiingereza.

1. Common Greetings – Salamu za kawaida
English
Kiswahili

Hello
Habari / Hujambo

Hi
Habari

Good morning
Habari za asubuhi

Good afternoon
Habari za mchana

Good evening
Habari za jioni

Good night
Usiku mwema

Kumbuka:
👉 Good morning hutumika asubuhi.
👉 Good afternoon hutumika mchana.
👉 Good evening hutumika jioni unapomsalimia mtu.
👉 Good night mara nyingi hutumika wakati wa kuagana au kwenda kulala

2. Asking about someone's condition
How are you? = Hujambo? / Ukoje?
Unaweza kujibu:
I am fine. = Niko vizuri.
I am very well. = Niko vizuri sana.
I am good. = Niko vizuri.
I am okay. = Niko sawa.
I am fine, thank you. = Niko vizuri, asante.

3. Short Conversation
A: Good morning!
B: Good morning!

A: How are you?
B: I am fine, thank you. How are you?
A: I am very well, thank you

4. Other useful expressions
Thank you = Asante.
You are welcome = Karibu / Usijali.
Goodbye = Kwaheri.
See you later = Tutaonana baadaye.
See you tomorrow = Tutaonana kesho.

✍️ Exercise
A. Translate into English:
1. Habari za asubuhi.
2. Ukoje?
3. Niko vizuri, asante.
4. Kwaheri.
5. Tutaonana kesho.

B. Complete the conversation:
A: Good morning!
B: ____________!

A: How are you?
B: ____________, thank you.

🏠 Homework
Andika mazungumzo mafupi ya Kiingereza kati ya watu wawili, ukitumia angalau maneno 5 tuliyojifunza leo.

Challenge: Jaribu kumsalimia mtu mmoja leo kwa Kiingereza. 😊

Karibu ujiunge na English academy tujifunze pamoja.

Introduce Yourself

 Introducing Yourself
 Kujitambulisha wewe mwenyewe

Katika somo hii utajifunza jinsi ya kujitambulisha kwa Kiingereza. Tutajifunza kusema jina lako, kazi yako, unakotoka na mambo machache kuhusu wewe.

What is your name?
 Jina lako nani?

My name is Jenicia.
Jina langu ni Jenicia.

What do you do?
 Unafanya kazi gani?

I am a teacher.
 Mimi ni mwalimu.

Where are you from?
Unatoka wapi?

I am from Tanzania.
 Ninatoka Tanzania.

🗣️ Dialogue - Mazungumzo

Person A: Hello!
Person B: Hello!

Person A: What is your name?
Person B: My name is Jenny.

Person A: What do you do?
Person B: I am a doctor.

Person A: Where are you from?
Person B: I am from Bukoba
.
Person A: Nice to meet you.
Person B: Nice to meet you too.

✍️ Practice
Jibu maswali haya kwa kutumia taarifa zako mwenyewe:

What is your name?
What do you do?
Where are you from?

Challenge 🎯
Andika mazungumzo mafupi kati ya Person A na Person B kwa kutumia maswali na majibu tuliyojifunza leo.
Usiogope kufanya makosa. Makosa ni sehemu ya kujifunza English.
 
Jenicia English Academy
Ifuatilie Jenicia English Academy kwa lessons zaidi za Beginner English zinazofundishwa kwa njia rahisi, kwa kutumia English na Kiswahili.

Karibu Jenicia English Academy (JEA)

Karibu Jenicia English Academy (JEA)
Tunayo furaha kukutangaza kuwa baada ya kipindi cha ukimya, tumerejea rasmi na utambulisho mpya

Learn English Language (LEL) sasa imebadilisha jina na kuwa Jenicia English Academy (JEA).

Mabadiliko haya yanaashiria mwanzo wa safari mpya yenye lengo la kuwasaidia wanafunzi, wafanyakazi, wafanyabiashara na kila anayependa kujifunza Kiingereza kwa njia rahisi, ya vitendo na yenye matokeo
.
Katika Jenicia English Academy (JEA) utapata:
Mafunzo ya Spoken English
English Grammar
Vocabulary (Msamiati)
Writing Skills (Uandishi wa Kiingereza)
Mazoezi, maswali na nyenzo mbalimbali za kujifunza

Dhamira yetu ni kukusaidia kujifunza Kiingereza kwa ufanisi ili ukitumie kwa kujiamini katika masomo, kazi, biashara na mawasiliano ya kila siku.
Kuanzia sasa tutakuwa tukichapisha masomo ya bure, vidokezo vya kujifunza Kiingereza, mazoezi, pamoja na taarifa kuhusu kozi zetu mbalimbali.

Ikiwa ulikuwa sehemu ya jamii yetu hapo awali, tunakushukuru kwa kuendelea kuwa nasi. Na kama ni mara yako ya kwanza kutembelea blog hii, karibu sana Jenicia English Academy.
Safari yetu inaanza leo. Tujifunze, tukue na tufanikiwe pamoja.

Jenicia English Academy (JEA)

Learn English, Transform Your Future

.📱 Jiunge na Kikundi Chetu cha WhatsApp Bure

Je, unataka kupata masomo ya bure ya Kiingereza, mazoezi, maswali, msamiati, vidokezo vya Grammar na taarifa za kozi zetu?
Karibu ujiunge na kikundi chetu cha WhatsApp cha Jenicia English Academy (JEA) na ujifunze pamoja na wanafunzi wengine kutoka maeneo mbalimbali.

Bonyeza link kujiunga.
https://chat.whatsapp.com/HGqqKlRReds00q1dKt9M2c

Karibu Jenicia English Academy (JEA). Tujifunze Kiingereza, tukue na tufanikiwe pamoja!

Welcom to Jenicia English Academy ( JEA )

After a period of being offline, I am excited to announce that our English learning community is back with a new identity.

Learn English Language (LEL) has now been rebranded as Jenicia English Academy (JEA).

This new name represents a bigger vision—to provide practical, high-quality English learning that helps students, job seekers, professionals, and anyone who wants to improve their English communication skills.

At Jenicia English Academy, you can expect:
Spoken English lessons
English Grammar
Vocabulary development
Writing skills

English for everyday communication
Learning materials, quizzes, and practice exercises
Our goal is simple: to make learning English practical, enjoyable, and effective.

Over the coming weeks, we will begin publishing new lessons, learning resources, and announcements about our upcoming training programs. If you have been following us before, thank you for your continued support. If you are new, you are warmly welcome to join our learning community.
This is just the beginning of a new journey.
Welcome to Jenicia English Academy (JEA).

Learn English, Transform Your Future.

📚 Join Our Free WhatsApp English Learning Community

Would you like to receive free English lessons, quizzes, vocabulary, grammar tips, and updates from Jenicia English Academy?

Click the link below to join our WhatsApp group:

👉https://chat.whatsapp.com/HGqqKlRReds00q1dKt9M2c?s=cl&p=a&ilr=0&amv=2

We look forward to learning English together!

PRESENT TENSE




Published from Blogger Prime Android App


PRESENT TENSE : WAKATI ULIOPO

Huu ni wakati ambayo hutumika kuelezea matukio yanayotokea sasa, Kila siku, Kila mwezi,matukio ya mara Kwa mara, ya mazoea na ya kawaida.

This tense used to explain the things/ action which happens everyday, weekly, monthly, often and always.

Namna Matendo Yanavyobadilika Kwenye Wakati Uliopo.
Kuna kanuni zimewekwa kurahisisha ubadilishaji wa matendo (action) kutoka mda Fulani kuingia mda mwingine.

Matendo yote yaliyomo katika present tense huongezwa " s" au "es" au "ies" yanapokuwa yamehusishwa na viwakilishi (pronouns) He,She,It.

Chunguza mifano ifuatayo.

Statement : Sentensi kamili

Verb :Come



1 .He comes here

Yeye Huwa anakuja hapa



2. She comes here

Yeye(she) Huwa anakuja hapa



3. It comes here

Yeye(it) Huwa anakuja hapa

Katika Sentensi hapo JUU kitenzi kimeongezwa "s" Kwa sababu Viwakilishi (he,she it) vimetumika hapo.

NB:Kumbuka Viwakilishi (I,We,They,you) kitenzi Huwa hakibadiliki Kwa namna yote Ile Wala kuongezewa kitu chochote.


1. We come here

Sisi Huwa tunakuja hapa


2. They come here

Wao Huwa wanakuja hapa


3.I come here

Mimi Huwa nakuja hapa


4. You come here

Wewe Huwa unakuja hapa



Itaendelea...........

Jiunge Katika Group Letu la Whatsup Kujifunza Kiingereza

Karibu msomaji wa Learn English Language. Leo nataka nikushauri Jambo mhimu sana, Kwa wale wanaotaka kujifunza kiingereza tuna group la Whatsup ambako Kuna uwanja Moana wa kujifunza kutoka kwa wengine, kuuliza maswalikatika group tunatumia audio na maandishi.

Kujiunga bonyeza kwenye link hii https://chat.whatsapp.com/HGqqKlRReds00q1dKt9M2c

Bonyeza hiyo link hapo juu kujiunga

Email : jeniciaj55@gmail.com
Phone: 0654221000