HII NDIO MISINGI YA KUJIFUNZA KUONGEA KIINGEREZA - ENGLISH SPEAKING BASICS






 English Speaking Basics ni misingi ya kujifunza kuongea lugha ya kiingereza,misingi hii imejumlisha maneno ya kiingereza yanayotumika katika maisha yetu ya kila siku.Kujifunza sarufi ya kiingereza kila siku inavunja moyo wa kuendelea kujifunza lakini kuanzia leo tutajifunza sarufi  na misingi ya kuongea kiingereza,unaweza kujikuta unaongea kiingereza kabla ya kumaliza kujifunza sarufi na ndipo ukaendelea kujifunza vizuri somo la sarufi.Karibu tujifunze msingi wa kwanza wa kujua kuongea kiingereza.

ENGLISH SPEAKING BASIC
 LESSON 1 : BASIC USAGE OF  I'AM - MATUMIZI YA "I'AM"

 "I'm " ni kifupisho cha I am.Inatumika kua kuambatanishwa na maneno mengine kumwambia mtu kuhusu wewe mwenyewe au kuelezea kitu au jambo unalofanya.

I'm is an abbreviation for the word ''I'AM".It is used in combination with other words to tell someone about yourself or to describe something you are doing.


EXAMPLES
  • I'm tired  - nimechoka
  • I'm happy - ninafuraha
  • I'm leaving work - naacha kazi
  • I'm thirsty - nina kiu
  • I'm 20 years old - nina miaka 20
  • I'm confused - nimechanganyikiwa
Vilivile unaweza kuongeza maneno mengine kuonesha msisitizo
Mfano
  • I am extremely tired - nimechoka sana
  • I am very happy - ninafuraha sana
  • I am very nervous - naogopa sana

Neno hili hutumika sana katika maisha yetu ya kila siku ndio sababu nikaliweka kuwa msingi wa wewe kuweza kuongea kiingereza .Msomaji wa LEARN ENGLISH LANGUAGE jiunge na mtamdao huu sasa ili uendelea kuwa na mimi katika masomo yanayofuata ambapo tutaendelea kujifunza misingi mingine mingi zaidi.Karibu tujifunze lugha ya kimataifa.

Your Tutor
Jenicia John
http://tlearningenglish.blogspot.com.
 

1 comment:

  1. Nayapataje haya mafundisho matamu, maana umeniacha najilamba tu

    ReplyDelete