Msomaji wa mtandao wa LEARN ENGLISH LANGUAGE karibu katika somo la leo ambapo tutajifunza aina za manemo( Parts of Speech ) ambazo hutumika katika lugha ya kiingereza.Aina hizi za maneno ndio husaidiana kutengeneza sentensi yenye kuleta maana kamili.Karibu tujifunze pamoja.
TODAY'S LESSON PLAN
* Maana ya aina za maneno - Mearning of parts of Speech
* Oroddha ya aina za maneno - Classification of parts of Speech
* Maana ya Nomino - Meaning of Noun
* Mifano ya majina - Examples of noun
* Misamiati ya leo - Tosday's Vocabularies
* Zoezi 3 - Exercise 3
* Hitimisho - Conclusion
PARTS OF SPEECH - AINA ZA MANENO
Haya ni maneno ambayo yanaweza kuwa majina ya watu,majina ya sehemu ,majina ya vitu,kuelezea zaidi vitu,kuelezea zaidi kuhusu watu,au sehemu.Pia hutumika kuelezea tendo lilivyofanyika na uhusiano wa maneno katika sentensi.Haya ni maneno ambayo kila moja lina kazi yake katika kukamilisha maana ya sentensi.
Kuna aina nane za maneno katika lugha ya kiingereza,nazo ni;
There are eight parts of speech in English Language,namely;
- Nouns - Nomino / majina
- Adjectives - Vivumishi
- Pronouns - Viwakilishi
- Verb - Vitenzi
- Adverb - vielezi
- Preposition - Vihusishi
- Conjuction - Viunganishi
- Interjection - Vihisishi
NOUNS - MAJINA
Noun is a word that names a person,a place,anything or an idear
Nomino ni jina la mtu,sehemu,kitu chochote au wazo.
Mfano
Tumejifunza kwamba nouns ni majina ya watu ,sehemu.kitu au wazo lolote
Majina ya watu
John
Neema
Michael
Mariana
julieth
Majina sehemu
Mwanza
Morogoro
Iringa
Uganda
Majina ya Vitu
Table - meza
Tree - mti
House - nyumba
Fertilizer - mbolea
Majina ya Mawazo
Politeness - ukarimu
Sickness - ugonjwa
Loneliness - upweke
Sadness - huzuni
Arrogance - ukorofi
TODAY'S VOCABULARIES
Vocabulary Pronounciation Meaning
Identify - aidentifai - tambua
Underline - andalain - pigia mstari
Ability - abilet - uwezo wa kufanya jambo
Abolish - abolish - kukomesha,piga marufuku
EXERCISE 3: ZOEZI 3
Identify by underlining all nouns in the following sentences
Tambua na pigia mstari majina yote katika sentensi zifuatazo.
- This book is not available in bookshops - kitabu hiki hakipatikani kwenye maduka ya vitabu
- Hapiness is the name of a girl - Hapiness ni jina la mschana
- Mwanza is a region - Mwanza ni Mkoa
- He came from Arusha - Yeye alikuja kutoka Arusha
- That car is mine - Ile gari ni yangu
Ndugu msomaji wa LEARN ENGLISH LANGUAGE tuishie hapo siku ya leo ambapo tumejifunza aina za maneno na kujua zaidi kuhusu NOUN kwa kutumia mifano.Noun inavipengele vyake navyo tutavichambua katika kipindi kinachofuata.Usichoke kujifunza,jifunze kila siku hapa upate kuongeza maarifa,Karibu tujifunze pamoja,kama una swali usisite kuuliza mwalimu wako atajibu maswali yako yote
Madam
Jenicia John
Email: jeniciaj55@gmail.com
What is the chemistry
ReplyDeleteAsante thanks
ReplyDeleteahsante sana inasaidia
ReplyDeleteBe blessed wandugu, mnafanya kingereza kiwe kama maji
ReplyDeleteIT GOOD EVER......
ReplyDeleteMAY THE FOUNDER OF THIS BE BLESSED
it's really helpful.. thanks 🤍
ReplyDeleteKazi nzuri, thank you
ReplyDeletekuna aina ngapi za nomino
ReplyDelete