COLLECTIVE NOUNS - NOMINO / MAJINA YA JUMLA






 Collective nouns ni moja ya aina za noun/majina ambayo yanahusika na majina ya jumla.Katika somo la leo tutajifunza maana ya majina ya jumla na mifano yake,pia tutajifunza moja ya misingi ya namna ya kujua kuongea kiingereza,bila kusahau zoezi la kujipima uelewa wako katika somo la leo.

COLECTIVE NOUNS - NOMINO / MAJINA YA JUMLA
Collective noun ni nomino inayohusisha majina ya makundi ya wanyama,watu na marundo ya vitu
Collective noun  is a name of groups or collection of animals,people or things

Hii inamaanisha mkusanyiko au rundo la vitu unapewa  jina moja,
Mfano team,class,committee,staff na mengine mengi.

1. Kundi la wanajeshi huitwa jeshi
    A group of solders is called army

2. kundi la waimbaji linaitwa kwaya
   A group of singers is called choir

3. Kundi la watu linaitwa umati wa watu
    A group of people is called crowd

4. Kundi la wakurugenzi linaitwa bodi
    A group of directors is called  board

5. Kundi la vitabu linaitwa makitaba
   A group of books is called library

6. Kundi la waalimu linaitwa wafanyakazi.
   A group of teachers is called staff.

ZOEZI  : EXERCISE
Tafuta maana ya haya majina ya jumla na uyaandike kwenye daftari lako ,unaweza kuyapata kwenye dictionary navitabu vya kiingereza.
 Find the meaning of these collective noun and write them in your exercise book.
  • Class
  • team
  • Committee
  • Flock
  • Forest
  • Crew
  • Troop
  • Board
  • Gang
  • Cluster
  • School
 Conclusion
 Jambo la msingi lisilokuwa na ubishi,jitahidi kujisomea kwa bidii mpaka uelewe lugha ya kiingereza ,fanya mazoezi ya kuandika,kuongea na kusoma wrewe mwenyewe unapokwama angalia mtu aliekaribu yako muulize atakusaidia unaweza pia kuwasiliana na mimi naweza kukusaidia vizuri kabisa,lengo langu wewe ujue lugha ya kimataifa.Karibu tujifunze pamoja .

Your Tutor
Jenicia John
http://tlearningenglish.blogspot.com

0 comments:

Post a Comment