Je Unavijua Viwakilishi Milikishi Vinavyotumika Katika Lugha Ya Kiingereza?



Karibu katika somo la leo ambapo tunaendelea kuweka juhudi katika kujifunza lugha ya kimataifa.Leo tutaendelea kujifunza sarufi ya lugha (Grammar),tutajifunza viwakilishi milikishi (Possessive Pronouns)
Karibu tujifunze pamoja.

Possessive Pronouns : Viwakilishi Milikishi
Hivi ni viwakilishi ambavyo vinaonesha umiliki wa kitu au vitu wa mtu yeyote au kitu chochote.Mfano wa maneno yanayoonesha umilikishi ni changu,chake.chao,chetu,vyetu n.k

Yafuatayo ni maneno yanayoonesha viwakilishi milikishi katika lugha ya kiingereza.

1. My / Mine : -angu
    Hiki ni kiwakilishi milikishi cha wewe mwenyewe

Mfano/Example
This is my book : Hiki kitabu ni changu
It  is mine : Ni changu
It is belongs to me :Ninakimiliki mimi

2. Your / Yours : -ako
  Hiki ni kiwakilishi milikishi cha nafsi ya pili,kinaweza wakilisha mtu mmoja au wengi,anaweza kuwa mwanamke au mwanaume au wote kwa pamoja.

Mfano /Example
That is your car : Ile ni gari yako
It is yours : Ni yako

3. Our /Ours : -etu
Hiki ni kiwakilishi milikishi cha wingi,kiwakilishi hiki kinaweza kuwakilisha kundi la wuatu wengi,wanaweza kuwa wanawake au wanaume au wote kwa pamoja.

Mfano / Example
This is our village : Hiki ni kijiji chetu
It is ours : Ni chetu

4. His : -ake
Kiwakilishi hiki huwakilisha umilikishi wa mwanaume tu.

Mfano /Example
This is John's shirt : Hili ni shati la John
This is his shirt : Hili ni shati lake
It is his : Ni lake

5. Her /Hers :-ake
Hiki ni kiwakilishi milikishi kinachowakilisha umilikishi wa mwanamke tu.

Mfano :Example
That is Mariana's house : Ile ni nyumba ya Mariana
That is her house : Ile ni nyumba yake
It is hers : Ni yake

6. Their /Theirs : -ao
Hiki ni kiwakilishi milikishi cha wingi,wanaweza kuwa wanaume kwa wanawake au wote kwa pamoja.

Mfano ?Example
That is their school. : Ile ni shule yao
It is theirs :Ni ya kwao.


Msomaji wa LEARN ENGLISH LANGUAGE hivyo ndio viwakilishi milikishi vinavyotumika katika lugha ya kiingereza.Tuendeelee kuwa pamoja katika masomo yanayofuata ili kujifunza zaidi.Kama hujajiunga na mtandao huu jiunge sasa kujifunza zaidi .Karibu tujifunze pamoja.

Your Tuto
Jenicia John
http://tlearningenglish.blogspot.com




   




Msingi Wa Tano Wa Kujifunza Kuongea Lugha Ya Kiingereza



Ni siku nyingine tena msomaji wa mtandao wa Learn English Language karibu katika somo la leo ambapo tunaendelea kujifunza msingi wa tano wa kujifunza kuongea lugha ya kiingereza.Leo tutajifunza matumizi ya maneno ambayo hutumika sana katika mazungumzo katika maisha yetu ya kila siku.Maneno hayo ni "Trying +To"

 Trying :Haya ni maneno ambayo mtu hutumia kumfahamisha mtu mwingine kwamba anajaribu kwa namna yoyote ile kukamilisha jambo fulani kwa bidii sana.Kwa kuongeza kitenzi "to" ni kuonesha nini hasa ambacho anajaribu kufanya.

Soma:Mbinu za kujifunza lugha ya kiingereza

Pronoun + Trying : These are grammatical words whichi a person use to inform someone else what he/she attempting to accomplish something.By adding the verb "to" is to point out what exactrly you are attempting to do.

Mfano/Example
I am trying to do an exercise everyday
Najaribu kufanya mazoezi kila siku.

 John is trying to find any job to do
 John anajaribu kutafuta kazi yoyote ya kufanya

Children are trying to learn things by themselves
Watoto wanajaribu kujifunza vitu wao wenyewe

I am trying to explain myself to the teacher but she doesnt want to understand me.
Najaribu kujieleza kwa mwalimu lakini hanielewi.

He is trying to work hard.
yeye anajaribu kufanya kazi kwa bidii.

Msomaji  penye nia pana njia endelea kuwa nami ili tuendelee kujifinza,na kama hujajiunga jiunge sasa na mtandao huu ili kujifunza zaidi.Karibu tujifunze pamoja.

Your Tutor
Jenicia John
http://tlearningenglish.blogspot.com



HIVI NDIO VIWAKILISHI VYA NAFSI KATIKA LUGHA YA KIINGEREZA



 Ni siku nyingine tena msomaji wa LEARN ENGLISH LANGUAGE napenda kukukaribisha katika somo la leo ambapo tutajifunza maana ya viwakilishi (pronouns) na viwakilishi vya nafsi (Personal Pronoun) vinavyotumika katika lugha ya kiingereza.Karibu tujifunze pamoja.

PRONOUN : KIWAKILISHI
Pronoun ni neno linalosimama badala ya jina/nomino.
Hii inamaanisha neno hilo linawakilisha jina,viwakilishi vinaweza kusimama badala ya jina la mtu,sehemu,vitu hata wazo.Matumizi ya viwakilishi hayaluhusu majina kuandikwa tena katika sentensi kwa sababu tayari kiwakilishi kimesha wakilisha jina.

Pronoun is a word that stand instead of noun.
This means that pronoun represents nouns.A pronoun can represent a name of  person,place,things or an idea.The use of pronoun does not allow to rename the noun which is represented or replaced in the sentence.

PERSONAL PRONOUNS : VIWAKILISHI VYA NAFSI
Personal Pronouns ni viwakilishi vinavyowakilisha nafsi za watu.Viwakilishi hivi vipo katoka mifumo tofauti kulingana na uwepo wa watu,idadi na jinsia.
Kuna nafsi ya kwanza umoja na wingi ( "I : mimi "and "WE : sisi")
kuna nafsi ya pili umoja na wingi ("you : wewe")
kuna nafsi ya tatu umoja na wingi ("she,he,it" and "They")

Katika lugha ya kiingereza person pronouns zimegawanyika katika makundi saba ambayo ni I,WE,YOU,SHE,HE,IT and THEY.

1. I : MIMI
    Hiki ni kiwakilishi cha nafsi ya kwanza umoja cha jina binafsi.Kiwakilishi hiki hutumika pale mtu         unapojizungumzia wewe mwenywe.Hii ndio sababu inaitwa nafsi ya kwanza umoja.

Mfano /Example
Mimi huwa naenda mjini kila siku
I go to town everyday

2. WE : SISI
    Kiwakilishi hiki ni cha nafsi ya kwanza wingi.Hutumika pale mtu anapozungumzia jambo na yeye anakuwa  mmoja wa wahusika wote.Husimamia majina ya watu wengi,wanaweza kuwa wanawake au wnaume au wote kwa pamoja.
  
    Mfano /Example
     Mimi,John na Neema tunaenda kanisani
     I,John and Neema are going to the church
     We are going to the church.
     Sisi tunaenda kanisani.
    

3. YOU :WEWE /NINYI
     Kiwakilishi hiki husimama badala ya jina moja au mengi,huwakilisha nafsi ya pili umoja na wingi,
     na hutumika kwa jinsia zote.Pia hutumika pale mtu unapomzungumzia mtu mwingine ndio maana
     inaitwa nafsi ya pili.
     
       Mfano /Example
        Wewe lazima ufanye kazi kwa bidii ili ufanikiwe
         You must work hard in order to succeed  

4. THEY : WALE /WAO.
    Kiwakilishi hiki husimamia majina ya watu wengi kwa pamoja wanaweza kuwa wanaume au
    wanawake au wote kwa pamoja.
   
    Mfano / Example
     Jenny na John wanasoma vitabu
     Jenny na John are reading books
     They are reading books

5. HE : YEYE
    Kiwakilishi hiki husimamia jina la wanaume tu.Badala ya kutumia jina la mwanaume yule kiwakilishi
    chake hutumika kiwakiliska jina.
    Mfano / Example
    John ni baba yangu , John huwa ni daktari
    John is my father,John is a doctor.
    He is my father,he is a doctor

6. SHE: YEYE
    Hiki ni kiwakilishi cha nafsi ya tatu umoja,huwakilisha jina la mwanamke tu.Ni nafsi ya tatu umoja
    kwa sababu tunamzungmzia mtu yule na yuko peke yake na jinsia ya kike.
   
Mfano / Example
Mariana ni mwalimu mzuri sana wa saikorojia.
Mariana is a good teacher of psychology.
She is a good teacher of psychology.

7. IT : Ni kiwakilishi kinasimamia majina ya vitu vyote isipokuwa majina ya watu.Lakini pia
          mtoto  mchanga hutumia kiwakilishi hiki.
         
          Mfano /Example
           Ile ni gari yangu,ninaimiliki mimi.
           That is my car,it is belongs to me.
            
          Gari imeibiwa         
          A car has stolen
          It has stolen


Msomaji wa mtandao wa LEARN ENGLISH LANGUAGE tutaendelea kujifanza viwakilishi vingine vinavyotumika katika lugha ya kiingereza.Endelea kuwa nasi  na kama hujajiunga na mtandao huu jiunge sasa ili kuweza kujifunza zaidi lugha ya kimataifa.

Your Tutor
Jenicia John
http://tlearningenglish.blogspot.com



 
     





MSINGI WA NNE WA KUJUA KUONGEA KIINGEREZA




 Karibu katika somo la leo tunaendelea kujifunza misingi mbalimbali ya kujua kuongea lugha ya kiingereza.Siku ya leo tutajifunza matumizi ya neno "going to".Namna linavyotumika katika mazungumzo yetu ya kila siku.Karibu tujifunze pamoja.

"Going to" ni neno ambalo hutumika kumwelezea mtu ulichopanga kufanya wewe au mtu mwingine kwa sasa au unachotarajia kufanya kwa baadae.

"Going to" is the grammatical word which used when you are telling someone what you are planning to do at the moment or in the near future.

Mfano : Example
I am going to work.
Naenda kufanya kazi

Neema is giong to prepare dinner
Neema ataandaa chakula cha usiku

I am going to stop drinking alcohol
Nitaacha kunywa pombe

Sherry is going to help her friend to find job
Sherry atamsaidia rafiki yake kutafuta kazi

Our teacher  is going to teach us Maths
Mwalimu wetu ataatufundisha Maths

I am going to stop smoking
Nitaacha kuvuta sigara

She is going to read all those books
Yeye atasoma vile vitabu vyote.



 EXERCISE : ZOEZI



Msomaji wa LEARN ENGLISH LANGUAGE tutaendelea kujifunza maneno mengi zaidi yanayotumika katika maisha yetu ya kila siku,hii ndio misingi ya kujua kujifunza kuongea lugha ya kiingereza.

Your Tutor
Jenicia John
http://tlearningenglish.blogspots.com


COUNTABLE AND UNCOUNTABLE NOUNS




Karibu katika somo la leo ambapo tutajifunza Countable nouns na Uncountable nouns.Somo la leo litatusaidia kuelewa majina ya vitu vinavyohesabika na visivyohesabika,haya yanaweza kuwa majina ya watu au majina ya vitu.Karibu tujifunze pamoja.

COUNTABLE NOUNS - MAJINA YANAYOHESABIKA
Countable nouns ni majina ya vitu ambavyo vinaweza kuhesabika.Majina haya yanaweza kuwekwa katika hali ya umoja na wingi.

Countable nouns are names of things which can be counted.These names can be categorized ino singular and plural.

Mfano:Example
  • cow - ng'ombe
  • tree - mti
  • house - nyumba
  • woman - mwanamke
  • man - mwanaume
  • book - kitabu
  • church - kanisa
  • student - mwanafunzi
Majina haya yote yapo katika hali ya umoja na yanaweza kuwa katika wingi.Kuna sheria na kanuni za kufuata katika kuweka majina ya vitu kwenye wingi,tutajifunza sheria hizo kwenye kipindi cha umoja na wingi.





UNCOUNTABLE NOUNS : MAJINA YASIYOHESABIKA
Uncountable nouns ni majina yavitu ambavyo havihesabiki ,wala hayawezi kuwa katika umoja na wingi.
Uncountable nouns are names of things which can not be counted or divided into singular and plural.

Mfano : Example
  • milk - maziwa
  • water - maji
  • rice - mchele
  • honey - asali
  • butter - siagi
  • flour - unga
  • sand - mchanga
NOTE: Vitu hivi vinawea kuwekwa kwenye hali ya wingi kama vitakuwa vimejazwa ndani ya vifaa vinginr.
             Mfano:
  •  three spoon of sugar - vijiko vitatu vya sukari
  • ten bottle of water - chupa kumi za maji
  • two bags of  rice - mifuko miwili ya mchele




TODAY'S VOCABULARIES : MISAMIATI YA LEO
Vocabulary/msamiati                         Pronounciation/matamshi                     Meaning/maana
accident                                           -aksident                                                  -tukio la ajari
acclaim                                            -akleim                                                     -pokea kwa shangwe
acclamation                                      -aklemeshen                                              -vegeregere,vifijo
accord                                              -akod                                                       - mapatano
accompany                                        -akampany                                               - fuatana na..,ongozana
accomplish                                        - akomplish                                                - timiza,tekeleza

Mwisho wa somo letu la leo,kama hujajinga na mtandao huu wa LEARN ENGLISH LANGUAGE jiunge sasa ili tuendelee kujifunza lugha ya kimataifa.kama umejiunga tuatumiwa email ya mafunzo kila siku kwr
enye email yako.Karibu tujifunze pamoja.

Your Tuto
Jenicia John
http://tlearningenglish.blogspot.com
         




                 

HUU NDIO MSINGI WA TATU WA KUJUA KUONGEA LUGHA YA KIINGEREZA



Habari msomaji wa LEARN ENGLISH LANGUAGE ni siku nyingine tena napenda kukukaribisha katika somo la leo ambapo tutajifunza msingi wa 3 wa kujua kuongea kiingereza,Msingi huu ni maneno ya kawaida kabisa ambayo yanatumika katika maisha yetu ya kila siku,leo tutajifinza matumizi ya neno "good at"

"GOOD AT"
Hili ni neno ambalo hutumika kuelezea uwezo wa mtu alionao katika kufanya jambo fulani kwa umakini wa hali ya juu kwa sababu yeye ni mtaalamu katika jambo lile.Angalia sentensi zifuatazo:

Mfano:
1. I am good at cooking
    Mimi ni mzuri sana katika mapishi
    Hii inamaanisha mimi nina uwezo mzuri sana katika kupika

2. Neema is good at dancing music
    Neema ni mzuri sana katika kucheza mziki

3.Children are good at playing football
   watoto ni wazuri sana katika kucheza mpira.

4. Asha is good at writting novel
    Asha ni mzuri sana katika uandishi wa riwaya

5. We are good at swimming
     Sisi ni wazuri sana katika kuogerea

6. They are good at conducting research
     Wao ni wazuri sana katika kufanya utafiti

7.John and Jack are good at driving a car.  
   John na Jack ni wazuri sana katika kuendesha gari.

8. Jenny is good at English Language and French
    Jenny ni mzuri sana katika lugha ya Kiingereza na Kifaransa

Sentensi hizi zote zinaonyesha watu hawa wanauwezo wa kufanya jambo fulani vizuri  kwa ufanisi na usahihi zaidi.Msomaji wa Learn English Language tutaendelea kujifunza maneno mengi zaidi ambayo yanatumika katika maisha yetu ya kila siku,maneno haya yanaweza kuwa mwongozo na msingi wa kujua kuongea lugha ya Kiingereza.Kama hujajiunga na muandao huu jiunge sasa tujifunze pamoja.

Your Tutor
Jenicia John
http:/tlearningenglish.blogspot.com

JE WAJUA ABSTRACT NOUNS?



 Jifunze lugha ya kimataifa uendane na maisha ya ulimwengu wa leo.Msomaji wa  LEARN ENGLISH LANGUAGE karibu katika somo letu la leo ambapo tutaendelea kujifunza sarufi ya kiingereza(Grammar).Bado tunachambua aina za majina (nouns) na leo tutajifunza zaidi kuhusu abstract nouns.

ABSTRACT NOUNS  - NOMINO / MAJINA DHAHANIA
Abstract nouns ni majina ya vitu visivyoonekanana huwa ni vitu vyakufikilika tu
Abstract nouns are names of quality,action or state that qualify ideas or state of mind.

Sifa za abstract nouns - Characteristics of abstract nouns
  • They are not physical things - hayana maumbo ya kuonekana
  • They can not be seen - havionekane kwa macho
  • They can not be heard - havisikiki 
  • They can not be smelt - havina harufu
  • They can not be touched -  havishikiki / huwezi kuvishika
Mifano ya nomino/majina dhahania - Examples of abstract nouns
  • kindness - wema
  • education - elimu
  • skills - ujuzi
  • love - upendo
  • dearth - kifo 
  • truth - ukweli
  • justice - haki
  • freedom -  uhuru
  • growth - ukuaji
  • liberty - uhuru
  • ability - uwezo 
  • sadness -  huzuni
  • cruelty - ukatiri
  • joy - furaha
  • obedience - utii
  • life - maisha


Haya ni baadhi ya majina ya kufikilika - these are few names of abstract nouns.
Hivyo endelea kujisomea zaidi utajua majina mengi sana ya dhahania (abstract nouns) Na hayo hapo juu kwenye jedwari jitahidi kutafuta maana ya kila neo ili kuongeza misamiati kichwani kwako,unaweza kupata maazake kwenye dictionary au unaweza kugoogle.

TODAY'S VOCABULARIES - MISAMIATI YA LEO
Vocabulary/mamiati                   Pronunciation/matamshi                            Meaning/maana
attrition                                    -atrishen                                                 - mvutano wa kimawazo
apath                                       - apas                                                    - kutojali
deception                                - disepshen                                             - udanganyifu
guess                                       - ges                                                       - dhania
sort                                         -sot                                                          - aina

Msomaji wa LEARN ENGLISH LANGUAGE somo letu la leo limefikia ukingoni,endelea kujifuza lugha ya kimataifa kwa kujiunga na mtanao huu jaza fomu ili kujiunga nasi ili utumiwe mafunzo haya moja kwa moja kwenye email yako.Karibu sana.

Your Tutor
Jenicia John
http://tlearningenglish.blogspot.com

MSINGI WA PILI WA KUJUA KUONGEA KIINGEREZA



Habari msomaji wa LEARN ENGLISH LANGUAGE karibu katika somo la leo ambapo tutajifunza msingi wa pili wa kujua kongea lugha ya kiingereza.Nauita ni msingi kwa sababu ni maneno ambayo yanatumika katika maisha yetu ya kila siku.Leo tutajifunza matumizi ya neno "I AM IN" na "I AM AT"

I AM IN - NIKO KWENYE AU NIKO NDANI YA...
Maneno haya hutumika kuelezea uko ndani ya kitu fulani au unaelezea jambo ambalo nafanya.
Angalia sentensi zifuatazo kujifunza zaidi;

1: I am in the school - Niko kwenye shule au niko shuleni
    Hii inamaanisha ndani ya shule

2: I am in the house - Niko kwenye nyumba
    Hii inamaanisha nimeingia ndani ya nyumba

3: I am in the kitchen - Niko jikoni
    Hii inamaanisha nimeingia ndani ya chumba cha kupikia/jikoni

4: I am in the box - Niko kwenye boksi
    Hii inamaanisha nimeingia ndani ya boksi

5: I am in the car - Niko kwenye gari
     Hii inamaanisha niko ndani ya gari




 "I am in the box" child said
  "Niko kwenye boks" Mtoto alisema







 

 One of them answered her phone said"i am in the car"


 Mmoja wao alijibu simu yake akasema "niko kwenye gari"




I AM AT - NIKO SEHEMU
Neno hili hutumika kumwelezea mtu sehemu ulipo  kwa wakati huo.
Mfano:
1. I am at the grocery - Niko kwenye mgahawa/
    Hii inamaanisha niko sehemu / maeneo ya mgahawa

2. I am at the airpot - Niko uwanja wa ndege
    Hii inamaanisha niko sehemu / maeneo ya uwanja wa ndege

3. I am at the Whitehouse - Niko Ikulu
    Hii inamaanisha niko sehemu au maeneo ya Ikulu
                       



 I am at beach
 Niko ufukweni mwa bahari (hii ni sehumu au eneo)







NOTE: Kuna wakati matumizi ya maneno haya yanaweza kukuchanganya,hebu angalia kwa makini sentensi zifuatazo zinafanana lakini zina maana tofauti kabisa;

1. I am in the supermarket.
2. I am at the supermarket.

Sentensi ya kwanza inamaanisha sehemu / eneo la supermarket.
Sentensi ya Pili inamaanisha niko ndani ya jengo la supermarket.

 3. I am at the police station.
 4. I am in the police station.

Sentensi ya kwanza namuelezea mtu kuwa niko sehemu /eneo la kituo cha polisi
Sentensi ya Pili namuelezea mtu kuwa niko ndani ya jengo la kituo cha polisi.

Somo letu la leo limeishia hapo,tutaendelea kujifunza zaidi misingi ya namna ya kujua kuongea kiingereza,endelea kufuatilia masomo yanayofuata,kama hujajiunga jiunge sasa na mtandao wa LEARN ENGLISH LANGUAGE ili kujifunza zaidi lugha ya kimataifa,Karibu tujifunze pamoja.

Your Tutor
Jenicia John
http://tlearningenglish.blogspots.com

    

   

CONCRETE NOUNS - NOMINO/MAJINA THABITI AU MGUSO




Msomaji wa LEARN ENGLISH LANGUAGE karibu katika somo la leo ambapo tutajifunza majina /nomino thabiti kwa  mifano,hii itatusaidia kujua majina thabiti ni majina ya vitu ambavyo vinaweza kuonekana au kuguswa.

CONCRETE NOUNS - MAJINA THABITI
Concrete noun ni jina la kitu thabiti chochote kinachoweza kuonekana kwa macho au kukigusa au hata kukitambua kwa harufu yake.
Concrete noun is a name of all things that can be seen or touched or can be identified by its smell.






Hii inamaanisha majina thabiti yamegawanyika katika makundi mawili:
1. Kuna majina thabiti ambayo yanaweza kuonekana na mengine kuweza kugusika
    Mfano
    kalamu - a pen
    kitabu - a book
    meza - a table
    nyumba - a house
    mti - a tree

2. Kuna majina thabiti ambayo hayaonekani na hayawezi kugusika 
    Mfano
    hewa - air
    hewa safi - oxygen
    hewa chafu - carbon dioxide




 TODAY'S VOCABULARIES - MISAMIATI YA LEO
Vocabulary/msamiati                     Pronounciation/matamshi                            Meaning/maana
absolute                                     - absolut                                                - kamili
abstain                                       - abstein                                                 -kujinyima,epukana na--
abstinence                                  - abstiens                                               - hali ya kujizuia kufanya jambo
abstruct                                      - abstrakt                                               - a kuwazika tu,dhahania
abstruction                                  - abstrukshen                                         - usahaurifu
      
Msomaji wa mtandao wa LEARN ENGLISH LANGUANGE tuishie hapa kwa siku ya leo,lakini enderea kujifunza lugha ya kimataifa .Kama hujajiunga na mtandao huu jiunge sasa ili uweze kutumiwa mafunzo haya kila siku.Karibu Tujifunze Pamoja.

Your Tutor
Jenicia John
hht://tlearningenglish.blogspot.com

HII NDIO MISINGI YA KUJIFUNZA KUONGEA KIINGEREZA - ENGLISH SPEAKING BASICS






 English Speaking Basics ni misingi ya kujifunza kuongea lugha ya kiingereza,misingi hii imejumlisha maneno ya kiingereza yanayotumika katika maisha yetu ya kila siku.Kujifunza sarufi ya kiingereza kila siku inavunja moyo wa kuendelea kujifunza lakini kuanzia leo tutajifunza sarufi  na misingi ya kuongea kiingereza,unaweza kujikuta unaongea kiingereza kabla ya kumaliza kujifunza sarufi na ndipo ukaendelea kujifunza vizuri somo la sarufi.Karibu tujifunze msingi wa kwanza wa kujua kuongea kiingereza.

ENGLISH SPEAKING BASIC
 LESSON 1 : BASIC USAGE OF  I'AM - MATUMIZI YA "I'AM"

 "I'm " ni kifupisho cha I am.Inatumika kua kuambatanishwa na maneno mengine kumwambia mtu kuhusu wewe mwenyewe au kuelezea kitu au jambo unalofanya.

I'm is an abbreviation for the word ''I'AM".It is used in combination with other words to tell someone about yourself or to describe something you are doing.


EXAMPLES
  • I'm tired  - nimechoka
  • I'm happy - ninafuraha
  • I'm leaving work - naacha kazi
  • I'm thirsty - nina kiu
  • I'm 20 years old - nina miaka 20
  • I'm confused - nimechanganyikiwa
Vilivile unaweza kuongeza maneno mengine kuonesha msisitizo
Mfano
  • I am extremely tired - nimechoka sana
  • I am very happy - ninafuraha sana
  • I am very nervous - naogopa sana

Neno hili hutumika sana katika maisha yetu ya kila siku ndio sababu nikaliweka kuwa msingi wa wewe kuweza kuongea kiingereza .Msomaji wa LEARN ENGLISH LANGUAGE jiunge na mtamdao huu sasa ili uendelea kuwa na mimi katika masomo yanayofuata ambapo tutaendelea kujifunza misingi mingine mingi zaidi.Karibu tujifunze lugha ya kimataifa.

Your Tutor
Jenicia John
http://tlearningenglish.blogspot.com.
 

COLLECTIVE NOUNS - NOMINO / MAJINA YA JUMLA






 Collective nouns ni moja ya aina za noun/majina ambayo yanahusika na majina ya jumla.Katika somo la leo tutajifunza maana ya majina ya jumla na mifano yake,pia tutajifunza moja ya misingi ya namna ya kujua kuongea kiingereza,bila kusahau zoezi la kujipima uelewa wako katika somo la leo.

COLECTIVE NOUNS - NOMINO / MAJINA YA JUMLA
Collective noun ni nomino inayohusisha majina ya makundi ya wanyama,watu na marundo ya vitu
Collective noun  is a name of groups or collection of animals,people or things

Hii inamaanisha mkusanyiko au rundo la vitu unapewa  jina moja,
Mfano team,class,committee,staff na mengine mengi.

1. Kundi la wanajeshi huitwa jeshi
    A group of solders is called army

2. kundi la waimbaji linaitwa kwaya
   A group of singers is called choir

3. Kundi la watu linaitwa umati wa watu
    A group of people is called crowd

4. Kundi la wakurugenzi linaitwa bodi
    A group of directors is called  board

5. Kundi la vitabu linaitwa makitaba
   A group of books is called library

6. Kundi la waalimu linaitwa wafanyakazi.
   A group of teachers is called staff.

ZOEZI  : EXERCISE
Tafuta maana ya haya majina ya jumla na uyaandike kwenye daftari lako ,unaweza kuyapata kwenye dictionary navitabu vya kiingereza.
 Find the meaning of these collective noun and write them in your exercise book.
  • Class
  • team
  • Committee
  • Flock
  • Forest
  • Crew
  • Troop
  • Board
  • Gang
  • Cluster
  • School
 Conclusion
 Jambo la msingi lisilokuwa na ubishi,jitahidi kujisomea kwa bidii mpaka uelewe lugha ya kiingereza ,fanya mazoezi ya kuandika,kuongea na kusoma wrewe mwenyewe unapokwama angalia mtu aliekaribu yako muulize atakusaidia unaweza pia kuwasiliana na mimi naweza kukusaidia vizuri kabisa,lengo langu wewe ujue lugha ya kimataifa.Karibu tujifunze pamoja .

Your Tutor
Jenicia John
http://tlearningenglish.blogspot.com

JE UNAYAJUA MAJINA YA KIPEKEE/MAALUMU? - PROPER NOUNS




 Katika somo la leo tutajifunza proper nouns (majina ya kipekee au maalumu),pia tutaangalia mifano ya proper nouns na kutakuwa na zoezi la kufanya kujipima umeelewa nini kuhusu proper nouns.karibu tujifunze pamoja.

 MAJINA YA KIPEKEE/MAALUMU - PROPER NOUNS
Proper nouns ni nomino inayohusisha majina ya watu,majina ya sehemu maalumu na majina ya vitu maalumu (particular things).Proper nouns zinapoandikwa kawaida huanza na herufi kubwa.Vilevile na siku za wiki na miezi huwa ni majina ya kipekee.

A proper noun refes toto the name of particular person,place,thing or an idear.When proper noun writen always begins with a capital letter.Aso days of the week and months of the year.

Mfano : Example
1. Majina ya watu -  Name of people
Nerson,Macha,John,jackob,Maganga

2. Majina ya sehemu maalumu - Name of particular location
Geita,Mwanza,kigoma,Tabora Railway Station,Dsm Bus Station

3. Majina ya vitu maalumu - Specific name
  • The Indian Ocean - Bahari ya Hinndi
  •  The Everest mountain - Mlima Everest
  • The God - Mungu
  • The moon - Mwezi
  • The Bible - Biblia
ZOEZI 5 :EXERCISE5
Find out buy underlining  proper nouns in the following sentences
Tambua kwa kupigia mstari majina maalumu katika sentensi zifuatazo

  1. Dodoma is the captal of Tanzania 
  2. America is a wealth Nation
  3. Mother Teresa was social worker
  4. History is the record of past events
  5. English is an Internation Language
TODAY'S VOCABULARIES - MISAMIATI YA LEO
Vocabulary / msamiati                      Pronounceation  / matamshi                          Meaning / maana             
  •  event                                    - ivent                                                      - tukio
  • social                                     -sosho                                                     - a jamii
  • particular                               - partikula                                               - maalumu
  • participate                              - participet                                                - shiriki
  • come                                      -kam                                                          - njoo
Asante kwa kuwa nami katka soma la leo,karibu tena katika somo linalofuata,kama una swali wasiliana na mwalimu wako atajibu maswali yako.Kama unaponda kuendelea kujifunza lugha ya kimataifa jaza fomu kujiunga nasi ili utumiwe email kila siku kupokea mafunzo haya.Karibu tujifunze pamoja

Your Tutor
Jenicia John
jeniciaj55@gmail.com









HIZI NDIO AINA ZA MAJINA - KINDS OF NOUNS

Msomaji wa LEARN ENGLISH LANGUAGE ni siku nyingine tena napenda kukukaribisha  katika somo la  leo ambapo tutajifunza aina za majina (kinds of nouns) zinazotumika katika lugha ya kiingereza.Karibu tujifunze pamoja.

TODAY'S LESSON PLAN
* Orodha ya aina za majina - Classification of nouns
* Maana ya majina ya kiwaida - Mearning of  common nouns
* Mifano ya majina ya kawaida - Examples of common nouns
* Misamiati  ya leo - Today's vocabularies
* Zoezi 4 - Exercise 4
* Conclusion - Hitimisho


ORODHA YA AINA ZA MAJINA - CLASSIFICATION OF NOUNS
Kuna aina nane za majina katika lugha ya kiingereza ambazo ni;
  1. Common nouns - Majina ya kawaida
  2. Proper nouns - Majina ya kipekee
  3. Collective nouns -Majina ya jumla
  4. Concrete nouns   - Majina yenye mguso/dhahili
  5. Abstruct nouns - Majina ya dhahania
  6. Countable nouns - Majina yenye kuhesabika
  7. Uncountable nouns - Majina yasiyohesabika
  8. materia nouns - majina ya mali harisia
Ili kuweza kuelewa aina hizi za najina tutajifunza kwa kuelezea moja baada ya nyingine,leo tutaanza na common nouns.

COMMON NOUNS - MAJINA YA KAWAIDA 

Majina ya kawaida ni majin ya kitu chochote kile isipokuwa majina ya watu..Majina haya hupatikana pote duniani,mara nyingi huanza na herufi ndogo isipokuwa kama litakuwa limetumika mwanzoni mwa sentensi ndipo litaanza kwa herufi kubwa.

common nouns are names of all things of the same class.

Mifano ya majina ya kawaida - Exemples of common nouns
  • boy - mvulana 
  • woman - mwanamke 
  • dog - mbwa
  • education - elimu
  • country - nchi
  • city - jiji
  • town - mji 
  • doctor - daktari
  • teacher - mwalimu
  • punishment - adhabu

soma:How Honest is the Key to Get Anything?


Ipo mifano mingi sana ya majina ya kawaida,cha msingi ni kuelewa kwamba common noun ni jina la kitu chochote kile kama tulivyoona hapo juu.

TODAY'S VOCABULARIES - MISAMIATI YA LEO
 Vocabulary                           Pronunciation (matamshi)                                 Meaning (maana)
above                                   -abavu                                                             -juu ya
abroad                                  -abroad                                                          -nchi za nje
abrogate                                -abrogeit                                                        -makubaliano
abrupt                                    -abrapt                                                           -gafula,-a kushitukiza
absence                                 - absens                                                          -hali ya mtu kutokuwepo         s
ZOEZI 4:EXERCISE 4
Make one sentense for each of the following common nouns.
Tengeneza sentensi moja kwa kila moja ya majina ya kawaida yafuatayo.
car,table,wisdom and carelessness.

CONCLUSION :HITIMISHO
Penye nia pana njia,msomaji wa LEARN ENGLISH LANGUAGE napenda kukuambia endelea kuweka jitihada katika kujisomea,usikate tamaa kijua lugha ya kimataifa,amini unaweza,twende pamoja mpaka ufanikiwe ulichodhamilia.Kama una swali usisite kuuliza mwalimu wako niko kwa ajili yako.

Your Tutor
Jenicia John
jeniciaj55@gmail.com
            












































ZIJUE AINA ZA MANENO - PARTS OF SPEECH



 Msomaji wa mtandao wa LEARN ENGLISH LANGUAGE karibu katika somo la leo ambapo tutajifunza aina za manemo( Parts of Speech ) ambazo hutumika katika lugha ya kiingereza.Aina hizi za maneno ndio husaidiana kutengeneza sentensi yenye kuleta maana kamili.Karibu tujifunze pamoja.


 TODAY'S LESSON PLAN
* Maana ya aina za maneno - Mearning of parts of Speech
* Oroddha ya aina za maneno - Classification of parts of Speech
* Maana ya Nomino - Meaning  of Noun
* Mifano ya majina - Examples of noun
* Misamiati ya leo - Tosday's Vocabularies
* Zoezi 3 - Exercise 3
* Hitimisho - Conclusion


PARTS OF SPEECH - AINA ZA MANENO
 Haya ni maneno ambayo yanaweza kuwa majina ya watu,majina ya sehemu ,majina ya vitu,kuelezea zaidi vitu,kuelezea zaidi kuhusu watu,au sehemu.Pia hutumika kuelezea tendo lilivyofanyika na uhusiano wa maneno katika sentensi.Haya ni maneno ambayo kila moja lina kazi yake katika kukamilisha maana ya sentensi.



CLASSIFICATION OF PARTS OF SPEECH
Kuna aina nane za maneno katika lugha ya kiingereza,nazo ni;
There are eight parts of speech in English Language,namely;
  1. Nouns - Nomino / majina
  2.  Adjectives - Vivumishi
  3. Pronouns - Viwakilishi
  4. Verb - Vitenzi
  5. Adverb - vielezi
  6. Preposition - Vihusishi
  7. Conjuction - Viunganishi
  8. Interjection - Vihisishi
Hizo ndio aina za maneno ambazo hutumika katika lugha  ya kiingereza kila moja ina vipengere vyake,kwa siku ya leo tutajifunza kipengele kimoja tu ambacho ni NOUNS (MAJINA)


NOUNS - MAJINA
Noun is a word that names a person,a place,anything or an idear
Nomino  ni jina la mtu,sehemu,kitu chochote au wazo.

Mfano
Tumejifunza kwamba nouns ni majina ya watu ,sehemu.kitu au wazo lolote
 Majina ya watu
John
Neema
Michael
Mariana
julieth

 Majina sehemu
Mwanza
Morogoro
Iringa
Uganda

Majina ya Vitu
Table - meza
Tree - mti
House - nyumba
Fertilizer - mbolea

Majina ya Mawazo
Politeness - ukarimu
Sickness - ugonjwa
Loneliness - upweke
Sadness - huzuni
Arrogance - ukorofi

 TODAY'S VOCABULARIES
 Vocabulary                               Pronounciation                         Meaning
Identify                 -                   aidentifai                         -        tambua
Underline             -                   andalain                          -        pigia mstari
Ability                  -                   abilet                              -        uwezo wa kufanya jambo
Abolish                -                   abolish                            -        kukomesha,piga marufuku

EXERCISE 3: ZOEZI 3
Identify by underlining all nouns in the following sentences
Tambua na pigia mstari majina yote katika sentensi zifuatazo.
  1. This book is not available in bookshops -  kitabu hiki hakipatikani kwenye maduka ya vitabu
  2. Hapiness is the name of a girl - Hapiness ni jina la mschana
  3. Mwanza  is a region - Mwanza ni Mkoa
  4. He came from Arusha - Yeye alikuja kutoka Arusha
  5. That car is mine  - Ile gari ni yangu
CONCLUSION   :  HITIMISHO
Ndugu msomaji wa LEARN ENGLISH LANGUAGE tuishie hapo siku ya leo ambapo tumejifunza aina za maneno na kujua zaidi kuhusu NOUN kwa kutumia mifano.Noun inavipengele vyake navyo tutavichambua katika kipindi kinachofuata.Usichoke kujifunza,jifunze kila siku hapa upate kuongeza maarifa,Karibu tujifunze pamoja,kama una swali usisite kuuliza mwalimu wako atajibu maswali yako yote

Madam
Jenicia John
Email: jeniciaj55@gmail.com











DEFINITE ARTICLE - KIBAINISHI DHIHIRISHI "THE"


TODAY'S LESSON PLAN
* Maana ya kibainishi dhihirishi - Meaning of definite article
* Matumizi ya definite article "the"
* Misamiati ya leo
* Zoezi 2
* Hitimisho-Conclusion

DEFINITE ARTICLE "THE" - KIBAINISH DHIHIRISHI "THE"
Kibainishi dhihirish ni kibainishi ambasho hutumikka kwenye maeneo maalamu.hii inamaanisha kwamba kile kitu kinachosimamiwa na kibainishi "the" kiwe kinaeleweka na kujulikana vizuri.


Mfano:
Nilimuona msichana jana alikuja hapa

I saw a girl came here yesterday.

Sentensi hii inaonesha haijulikani ni mschana gani alikuja jana,ndio sababu kibainishi "a" kimetumika.Angalia sentensi inaayofuata:

I saw the girl who used to prepare meal for us came here yesterday.
Nilimuona msichana ambae huwa anatuandalia chakula alikuja hapa jana.

Hapa tunaongelea mschana  maalumu ambae anajulikana ndio sababu kibainishi "the" kimetumika

Mfano 2
This is a house
Hii ni nyumba



 
 This is the house where I live
  Hii ni nyumba ambayo naishi

  • Sentensi ya kwanza  kibainishi "a"kimetumika kwa sababu ile ni nyumba ambayo hatuelewi undani wake,hatujui ni ya nani.

  • Sentensi ya pili kibainishi" the"kimetumika kwa sababu hii ni nyumba inayojulikana ni ya nani na nani anaishi pale.

USES OF DEFINITE ARTICLE "THE"- MATUMIZI YA KIBAINISHI KIDHIHIRISHI "THE"
1. Unique things Vitu vya kipekee

Kibainishi hiki hutumika kubainisha vitu vya kipekee.
Mfano:
The Sun - Jua
The sea - Bahari
The sky - Anga
The moon - Mwezi
The Earth - Dunia

2. Particular persons or things - Watu au vitu maalumu vinavyojulikana.

Mfano
The man you met yesterday is my ancle.
Mwanaume uliekutana nae jana ni mjomba wangu.

3. Persons or things mentioned for second time - Watu au vitu vinapotajwa kwa mara ya pili .
Mfano
I bought a car .The car was expensive.
Nilinunua gari.Gari ilikuwa ya gharama.

Katika sentensi hii jina "car" limetajwa mara mbili,ilipotanjwa mara ya kwanza kibainishi "a" kimetumika na ilipotajwa mara ya pili kibainishi "the" kimetumika.

4. Singular noun representing the whole class - Jina moja linalowakilisha kundi zima

Mfano
The teacher should know the psychology of the student.
Mwalimu anapaswa kumjua mwanafunzi kisaikolojia.
Sentensi hii inamaanisha walimu wote wanapaswa kuwajua vizuri wanafunzi kisaikolojia

5. Name of rivers,mountains,oceans - Majina ya mito,milima na bahari
 Majina haya hubainishwa na kibainishi dhihirishi "the"

Mfano
The Everest
The Pacific Ocean
The Indian Ocean

6. Well known books - Vitabu  vinavyojulikana sana
Kuna vitabu vinajulikana sana duniani kotea kiasi kwamba mtu yeyote wa taifa lolote ukimtajia ataelewa unazungumzia kitabu gani,vitabu hivi hubainishwa na kibainishi dhihirishi "the" .
Mfano
The Bible
The Koran


7. Adjective used as noun - Kivumidhi kinapotumika kama jina
Mfano
The rich - Tajiri
The poor  - Masikini
The strong - Chenye nguvu
The weak  - Dhaifu

8.Direction
"The"hutumika kubainisha pande za Dunia
Mfano
The North  - Kaskazinii
The South - Kusini
The East - Mashariki
The West - Magharibi

TODAY'S VOCABOLARIES - MISAMIATI YA LEO
Vocabolary             Pronounciation                 Meaning
Abbreviate            - abriviet                    -      Fupisha
Abbreviation           - abrivieishen            -      Ufupisho
Abdicate                 - abdikeit                  -    Jihudhuru
Abduct                    - abdakt                   -     Kuteka
Abductee               -  abdaktii                  -      Mateka(alietekwa)
Abductor                - abdakta                   -       Mtekaji

 EXERCISE : ZOEZI
Fill in the blanks with suitable article:a ,an or the.
Jaza nafasi zilizowazi kwa kibainishi sahihi: a,an or the
  1. My friend is ...................European
  2. We read .................... Bible
  3. Srilankais .................Island
  4. Jenny bought ................umbrella
  5. Mariana gave me ..............flower
CONCLUSION  - HITIMISHO
Kuna matumizi mengi sana ya kiambishi dhihirishi "the" ,tutaendelea kujifunza kadiri somo linavyoendelea.Cha msingi ni kuyafanyiakazi yale unayojifunza na kuweka bidii kubwa katika kujifunza hakika utafanikiwa kujua lugha ya kimataifa.Jizoeshe kusoma vitabu vya kiingereza utapata maarifa na kuendelea kujifunza zaidi

Your Tutor
Jenicia John
tlearning.blogspot.com
 


ARTICLES - VIBAINISHI VINAVYOTUMIKA KATIKA LUGHA YA KIINGERZA


 TODAY'S LESSON PLAN
* Maana ya Vibainishi - Meaning of Articles
* Aina za Vibainishi -Kind of Articles
* Matumizi ya Vibainishi - Uses of Article
* Misamiati ya leo - Today's Vocabolaries
* Zoezi - Exercise
* Hitimisho - Conclusion.

Habari za leo msomaji wetu natumaini unaafya njema kabisa ndio maana unaendelea kuweka jitihada kubwa katika kuendelea kujifunza lugha ya kiingereza pamoja na sisi.Tuko hapa kuhakikisha unaelewa na kuweza kutumia lugha hii kwa ufasaha na ufanisi zaidi. Karibu ndugu msomaji katika somo la leo ambapo tutajifunza vibainiahi vinavyotumika katika lugha ya kiingereza.Katika lugha ya kiingereza hasa majina ya vitu hutanguliwa na neno lingine kabla halijatamkwa,neno hilo huitwa kibainishi (Article)


VIBAINISHI - ARTICLES
Vibainishi ni maneno yanayowekwa kabla ya majina ili kuyabainisha.Vibainishi hinyo ni "A","AN" na "THE".
Articles are words placed before nouns to identify them.Articles include "A", "AN" and  "THE".

Mfano:
A tree
AN Orange
THE Bible
 kutoka kwenye hiyo mifano mitatu hapo juu tutapata aina za vibainishi

AINA ZA VIBAINISHI - KINDS OF ARTICLES.
Kuna aina mbili za vibainishi - There are two kinds of articles
  1. Indefinite Articles - Vibainishi visivyo dhihirishi
  2. Definite Article - kibainishi dhihilishi

1. INDEFINITE ARTICLES:"A","AN" - VIBAINISHI VISIVYO DHIHIRISHI "A","AN"
Hivi ni vibainishi vinavyo simama mwanzoni mwa majina yote yenye maana ya kitu kimija chochote.Hii inamaanisha kwamba vibainishi hivi  haviwezi kusimamia majina yaliyo katika hali ya wingi.
Vinaitwa vibainishi visivyo dhihirishi kwa sababu vinasimamia jina la kitu chochote kile bila ya kueleza kwa undani kuhusiana na kitu kile.Angalia sentensi inayofuata:

I saw John carring a book  -  Nilimuona John amebeba kitabu.

Katika sentensi hii John alionekana amebeba kitabu lakini haijulikani kile ni kitabu gani?,cha nini? .Ndio sababu kibainishi "a" kinetumika hapo haijulikani John alikuwa amebeba kitabu gani hakuna anaeweza kudhihirisha ila kile kilikuwa ni kitabu tu.

 NOTE:Vibainishi hivi hutofautiana matumizi kutokana na matamshi ya majina vinayoyasinamia,chunguza sentensi zifuatazo:
  1. "A" Kibainishi hiki husimamia majina yanayoanza na konsonanti tu,pia huweza kusimamia majina yanayoanza na irabu inapotamkwa kama konsonanti.
           Mfano:Example
 A  table - meza
A house - nyumba
A car - gari
A Uniform - sare
A Universal - ulimwengu

Katika hiyo mifano hapo juu mfano wa kwannza mpaka wa tatu,a table,a house,a car,haya yote ni  majina yanayoanza na konsonanti na yote yako katika hali ya  umoja ndio maana article "a" imetumika.kuvibainisha na matamshi yake yanaanza na konsonant.Na katika mfano wa nne na tano,a Uniform,a Universal,haya yote ni majina yanayoanza na irabu lakini katika matamshi inatoka sauti ya konsonanti.

a table         - e tebo
a house       - e haus
a car           - e kaa
a Uniform    - e  juniform
a Universal   - e juniverso

2. "AN"  Kibainishi hiki husimama katika majina yanayoanza na irabu tu,na majina yanayuanza na konsonati zinazotamkwa kama irabu..
Mfano:
An hour - en awa
An orange  - en orenji
An honest citizen  - en onest citizen

MISAMIATI YA LEO - TODAY'S VOCABULARIES.
Kila siku tutajifunza misamiati 5,matamshi na maana yake.

Msamiati                 -      Matamshi(pronounciation)                  -              Maana(meaning)
  • Abandon        -                             -                                       -              telekeza
  • Abandoned     -                             -                                        -              telekezwa
  • Abandoning     -                            -                                         -              kuacha
  • Abesemeny      -                   abeziment                                    -              fedheha
  • Abash                                            -                                         -              aibisha

EXERCISE - ZOEZI
1. Andika maneno 10  ya kiingereza yalnayotanguliwa na kibainishi "a"
2. orodhesha maneno 10 yanayotanguliwa na kibainishi "an"

Conclusion - Hitimisho
 Kujua vema vibainishi visivyo dhihilishi soma vitabu vya kiingereza na chunguza kwa makini sehemu ambayo vibainishi hivyo vimetumika .Utagundua mambo mengi sana kwa njia hii ya kujisomea mwenyewe.Kama unaswali lolote usisite kuuliza Mwalimu niko kwa ajili yako ni furaha yangu kuona unajua lugha ya kimataifa.
Karibu tujifunze pamoja.

Your Tutor
JENICIA JOHN
http://tlearningenglish.blogspot.com                   







HUU NDIO MUUNDO WA LUGHA YA KIINGEREZA.


INTRODUCTION -UTANGULIZI.

Ndugu msomaji karibu sana katika somo hili la leo ambapo ni muhimu sana kabla ya kujifunza sarufi (grammar),kujua lugha ni nini?,ni vitu gani vinaunda lugha?,kwa nini tunapaswa kujifunza lugha na kwa namna gani tunaweza kujifunza lugha.Ulimwenguni pote kuna lugha nyingi sana na kiingereza ni moja wapo,ambayo inajulikana kama lugha ya kimataifa.Hii ni kwa sababu mataifa mengi duniani kiingereza kinatumika katika shughuri mbalimbali,kwa mfano kazini,shuleni na hata kwenye biashara zetu.

 Inakuwa njia rahisi sana kujifunza kiingereza kwa kutumia lugha yetu ya taifa (KISWAHILI).Karibu tujifunze pamoja.

Lugha ni nini?- What is Language?
Lugha ni mfumo wa sauti wa sauti zinazotumiwa na watu  wa jamii fulani katika mawasiliano.
Language is the system of communication used by people of particular society.

Kwa nini tunajifunza Lugha? - Why we learn language?
Tunajifunza lugha ili itumike katika mawasiliano katika maisha yetu ya kila siku.
We learn language as means of communication in our daily life.

MUUNDO WA LUGHA.
Lugha imeeundwa kwa kwa herufu 26 tu,na herufi hizi zimegawanyika katika makundu mawili:
1.) konsonants/herufi bubu - Consonants
Kuna consonants 21 zinazotumika katika lugha ya kiingerza,na ziko katika herufi kubwa na ndogo kama ifuatavyo:
Bb,Cc,Dd,Ff,Gg,Hh,Jj, Kk,Ll,Mm,Nn,Pp,Qq,Rr,Ss,Tt,Vv,Ww,Xx,Yy,Zz.

2.)Irabu/Vokali  - Vowel
 Kuna herufi tano tu zinazojulikana kama Irabu..Aa,Ee,Ii,Oo,Uu.
Katika kujifunza lugha ili uweze kupata neno ni lazima pawepo na muunganiko wa konsonantis na irabu ili kupata neno kamili,konsonanti husumama kama baba na irabu husimama kama mtoto.

  • Word is the proper combination of letters  
           Neno ni muunganiko wa herufi.                    Mfano:
           Neno NATION limeunndwa kwa consonants na vowel..
  • Sentence is the group of words or word which has complete meaning.
           Sentesi ni kundi la maneno au neno lenye kuleta maana kamili.
  • Grammar is the scientific learning of language                                             
           Sarufi ni sayansi  inayotumika kujifunza lugha

Sarufi hutusaidia kuelewa namna lugha inavyoongewa na kuandikwa kwa usahihi na ufanisi zaidi.
Grammar helps us to understand how language is spoken and written in correctly and effectively way.

Hivyo basi Sarufi/grammar inahusika moja kwa moja. katika utungaji wa maneno katika lugha na mgawanyiko wa maneno,sentensi na matumizi yake katika maisha yetu ya kila siku.Kwa leo tuishie hapa usikose somo linalofuata amapo tutajifunza aina za maneno zinazotumika katika lugha ya kiingereza,endelea kuweka jitihada katika kujifunza.

Your Tutor
Jenicia John
Email : jeniciaj55@gmail.com