Hivi Ndivyo Unavyoweza Kujifunza Lugha Ya Kiingereza




Ndugu msomaji leo napenda tujifunze ni kwa namna gani mtu anaweza kujifunza lugha ya kiingereza.Kuna mbinu mbalimbali ambazo mtu anaweza kuzitumia kujifunza lugha yoyote.Kiingereza ni lugha ya kawaida kabisa ambayo mtu anaweza kujifunza na kujua kusoma,kuandika na kuongea bila tatizoKaribu tujifunze pamoja mbinu mbalimbali za kujifunza kiingereza.

1.Jiamini -Be Confindence.
Amini kwamba unaweza kujifunza na ukajua kusoma,kuandika na kuongea kiingereza,utaweza bila shaka kwanza kwa sababu unaamini unaweza,na usikate tamaa mapema jitahidi kila siku jifunze kwa kujiamini kwamba unaweza.

2.Kuwa na malengo - You must have goals
Ili uweze kujua lugha ya kiingereza lazima uweke malengo,na hakikisha lengo lako la kujua kiingereza linatimia kwa kwa kuwa na dhamila kwamba lazima ujue kusoma,kuandika na kuongea kiingereza lazima utafanikiwa tu.

3,Amini kwamba unaweza -Trust that you can do it
Katika hatua ya kujifunza yapo mambo mengi yatakukatisha tamaa ikiwa pamoja na kuona aibu watu watakufikiliaje au watakuonaje hujui kiingereza au unaongea unakosea wakucheka usikate tamaa amini kwamba unaweza sababu wote wanaoweza kuandika,kuongea na kusoma walijifunza tu,hivyo basi na wewe jifunze hakika unaweza,

4.Jifunze misamiati mipya kila siku - Learn new vocabularies everyday.
Hakikisha kila siku unajifunza misamiati au maneno mapya,jitahidi angalau jifunze maneno matano (5) kila siku,jifunze maana ya kila neno,jua kubadilisha katika nyakati,wakati uliopo,timilifu,endelevu,uliopita na wakati ujao.Hapa utakuta neno moja linamaana moja lakini linabadikika kulingana na nyakati..Tutajifunza huko mbele namna ya kubadilisha maneno katokana na mabadiliko ya nyakati.

5.Soma vitabu mbalimbali ili kujifunza maneno mapya- Read different books so as to learn new words
 Hakikisha unasoma vitabu vya kiingereza utajifunza maneno mapya mengi sana.Tafuta daftari la kuandikia maneno yote usiyoyajua (vocabularies) jitahidi utafute maana zake na uandike ili iwe rahisi kujisomea mpaka uyajue vizuri tunza vizuri hilo daftali utasaidia na wengine.

6.Angalia tamthilia za kiingereza -Watch movies in which they speak Englishi Language.
Hapa utajifunza namna ya kuongea na kutamka maneno ya kiingereza,amini ninachokuambia utaongea kiingereza kizuri sana.

7.Fanya mazoezi ya kuongea,kusoma na kuandika.-Do practice on speaking,reading and writting
 Jitahidi kufanya mazoezi ya kuongea,kusoma na kuandika japo utakosea na wengine kukucheka usikate tamaa,endelea kujifunza kwa bidii.

Niamini mimi kwa hakika unaweza weka jitihada kubwa utafanikiwa tu.Karibu ujiunge na mtanda huu tujifunze panoja lugha ya kimataifa.Tukutane tena siku nyingine kwenye  sehemu nyingine ya somo letu katika mtandao wa LEARN ENGLISH LANGUAGE.

Your Tutor
Jenicia John
tlearningenglish.blogspots.com
jeniciaj55@gmail.com

.

0 comments:

Post a Comment