HUU NDIO MUUNDO WA LUGHA YA KIINGEREZA.


INTRODUCTION -UTANGULIZI.

Ndugu msomaji karibu sana katika somo hili la leo ambapo ni muhimu sana kabla ya kujifunza sarufi (grammar),kujua lugha ni nini?,ni vitu gani vinaunda lugha?,kwa nini tunapaswa kujifunza lugha na kwa namna gani tunaweza kujifunza lugha.Ulimwenguni pote kuna lugha nyingi sana na kiingereza ni moja wapo,ambayo inajulikana kama lugha ya kimataifa.Hii ni kwa sababu mataifa mengi duniani kiingereza kinatumika katika shughuri mbalimbali,kwa mfano kazini,shuleni na hata kwenye biashara zetu.

 Inakuwa njia rahisi sana kujifunza kiingereza kwa kutumia lugha yetu ya taifa (KISWAHILI).Karibu tujifunze pamoja.

Lugha ni nini?- What is Language?
Lugha ni mfumo wa sauti wa sauti zinazotumiwa na watu  wa jamii fulani katika mawasiliano.
Language is the system of communication used by people of particular society.

Kwa nini tunajifunza Lugha? - Why we learn language?
Tunajifunza lugha ili itumike katika mawasiliano katika maisha yetu ya kila siku.
We learn language as means of communication in our daily life.

MUUNDO WA LUGHA.
Lugha imeeundwa kwa kwa herufu 26 tu,na herufi hizi zimegawanyika katika makundu mawili:
1.) konsonants/herufi bubu - Consonants
Kuna consonants 21 zinazotumika katika lugha ya kiingerza,na ziko katika herufi kubwa na ndogo kama ifuatavyo:
Bb,Cc,Dd,Ff,Gg,Hh,Jj, Kk,Ll,Mm,Nn,Pp,Qq,Rr,Ss,Tt,Vv,Ww,Xx,Yy,Zz.

2.)Irabu/Vokali  - Vowel
 Kuna herufi tano tu zinazojulikana kama Irabu..Aa,Ee,Ii,Oo,Uu.
Katika kujifunza lugha ili uweze kupata neno ni lazima pawepo na muunganiko wa konsonantis na irabu ili kupata neno kamili,konsonanti husumama kama baba na irabu husimama kama mtoto.

  • Word is the proper combination of letters  
           Neno ni muunganiko wa herufi.                    Mfano:
           Neno NATION limeunndwa kwa consonants na vowel..
  • Sentence is the group of words or word which has complete meaning.
           Sentesi ni kundi la maneno au neno lenye kuleta maana kamili.
  • Grammar is the scientific learning of language                                             
           Sarufi ni sayansi  inayotumika kujifunza lugha

Sarufi hutusaidia kuelewa namna lugha inavyoongewa na kuandikwa kwa usahihi na ufanisi zaidi.
Grammar helps us to understand how language is spoken and written in correctly and effectively way.

Hivyo basi Sarufi/grammar inahusika moja kwa moja. katika utungaji wa maneno katika lugha na mgawanyiko wa maneno,sentensi na matumizi yake katika maisha yetu ya kila siku.Kwa leo tuishie hapa usikose somo linalofuata amapo tutajifunza aina za maneno zinazotumika katika lugha ya kiingereza,endelea kuweka jitihada katika kujifunza.

Your Tutor
Jenicia John
Email : jeniciaj55@gmail.com

Hivi Ndivyo Unavyoweza Kujifunza Lugha Ya Kiingereza




Ndugu msomaji leo napenda tujifunze ni kwa namna gani mtu anaweza kujifunza lugha ya kiingereza.Kuna mbinu mbalimbali ambazo mtu anaweza kuzitumia kujifunza lugha yoyote.Kiingereza ni lugha ya kawaida kabisa ambayo mtu anaweza kujifunza na kujua kusoma,kuandika na kuongea bila tatizoKaribu tujifunze pamoja mbinu mbalimbali za kujifunza kiingereza.

1.Jiamini -Be Confindence.
Amini kwamba unaweza kujifunza na ukajua kusoma,kuandika na kuongea kiingereza,utaweza bila shaka kwanza kwa sababu unaamini unaweza,na usikate tamaa mapema jitahidi kila siku jifunze kwa kujiamini kwamba unaweza.

2.Kuwa na malengo - You must have goals
Ili uweze kujua lugha ya kiingereza lazima uweke malengo,na hakikisha lengo lako la kujua kiingereza linatimia kwa kwa kuwa na dhamila kwamba lazima ujue kusoma,kuandika na kuongea kiingereza lazima utafanikiwa tu.

3,Amini kwamba unaweza -Trust that you can do it
Katika hatua ya kujifunza yapo mambo mengi yatakukatisha tamaa ikiwa pamoja na kuona aibu watu watakufikiliaje au watakuonaje hujui kiingereza au unaongea unakosea wakucheka usikate tamaa amini kwamba unaweza sababu wote wanaoweza kuandika,kuongea na kusoma walijifunza tu,hivyo basi na wewe jifunze hakika unaweza,

4.Jifunze misamiati mipya kila siku - Learn new vocabularies everyday.
Hakikisha kila siku unajifunza misamiati au maneno mapya,jitahidi angalau jifunze maneno matano (5) kila siku,jifunze maana ya kila neno,jua kubadilisha katika nyakati,wakati uliopo,timilifu,endelevu,uliopita na wakati ujao.Hapa utakuta neno moja linamaana moja lakini linabadikika kulingana na nyakati..Tutajifunza huko mbele namna ya kubadilisha maneno katokana na mabadiliko ya nyakati.

5.Soma vitabu mbalimbali ili kujifunza maneno mapya- Read different books so as to learn new words
 Hakikisha unasoma vitabu vya kiingereza utajifunza maneno mapya mengi sana.Tafuta daftari la kuandikia maneno yote usiyoyajua (vocabularies) jitahidi utafute maana zake na uandike ili iwe rahisi kujisomea mpaka uyajue vizuri tunza vizuri hilo daftali utasaidia na wengine.

6.Angalia tamthilia za kiingereza -Watch movies in which they speak Englishi Language.
Hapa utajifunza namna ya kuongea na kutamka maneno ya kiingereza,amini ninachokuambia utaongea kiingereza kizuri sana.

7.Fanya mazoezi ya kuongea,kusoma na kuandika.-Do practice on speaking,reading and writting
 Jitahidi kufanya mazoezi ya kuongea,kusoma na kuandika japo utakosea na wengine kukucheka usikate tamaa,endelea kujifunza kwa bidii.

Niamini mimi kwa hakika unaweza weka jitihada kubwa utafanikiwa tu.Karibu ujiunge na mtanda huu tujifunze panoja lugha ya kimataifa.Tukutane tena siku nyingine kwenye  sehemu nyingine ya somo letu katika mtandao wa LEARN ENGLISH LANGUAGE.

Your Tutor
Jenicia John
tlearningenglish.blogspots.com
jeniciaj55@gmail.com

.

LUGHA YA KIMATAIFA.


KARIBU TUJIFUNZE PAMOJA.

English Language ni lugha ya kimataifa ambayo inatumika katika maisha yetu ya kila siku.Dunia inabadilika na kila kitu kinabadilika hivyo basi ni vyema na sisi tukaendana na hayo mabadiliko ya sayansi na tekinolojia.Lugha ya kiingereza inaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa watu wakaishi maisha mazuri kabisa.Hii ni kwa sababu lugha hii inatumika kazini,shuleni na hata kwenye biashara zetu,kama mtu anaelewa kuandika,kusoma na kuongea kiingereza itamsaidia sana katika shughuli za kila siku.
 kama unapenda kujifunza lugha ya kiingereza  karibu tujifunze pamoja

JENICIA JOHN
jeniciaj55@gmail.com
0654 221 000