Msomaji wa Learn English Language karibu katika somo letu la leo ambapo tutajifunza kitenzi (verb) katika lugha ya kiingereza.Vitenzi ni maneno ambayo yanatumika sana katika mazungumzo yetu ya kila siku inaweza kuwa nyumbani,kazini,shuleni au sehemu yoyote.
(a) What is a Verb?
Kitenzi ni nini?
Verb is a word which used to indicate an action,a state of being existence or possession.
itenza ni neno ambalo hutumika kuonesha kitendo,hali ya uwepo wa jambo au umiliki wa kitu.
mfano : example
I speak English : Ninaongea kiingereza
She works hard : Yeye hufanya kazi kwa bidii
Juma plays football : Juma hucheza mpira.
NOTE: Maneno yote yaliyopigiwa mstari ni vitenzi (Verbs)
(b) Uses of Verbs: Matumizi Ya Vitenzi
1.Verb used to tell us what a person or a thing does.
Kitenzi hutumika kutuambia nini mtu anafanya au kitu gani kinafanya nini.
Mfano : examples
Michael writes novel : Michael huwa anaandika hadidhi.
Sentensi hii inaonesha Michael huwa anafanya tendo la kuandika hadidhi.
The Sun rises everyday : Jua huchomoza kila siku
2. Verbs tells us what is done to a person or a thing
Kitenzi hutumika kutuambia tendo alilofanyiwa mtu au kitu.
Mfano : Example
He has punished :Yeye ameadhibiwa
Sentensi hii inaonesha mtu (he) amefanyiwa kitendo cha kuadhibiwa
3.Verb tells us about a state of being or existence.
Kitenzi hutuambia hali ya mtu au uhalisia wake.
Mfano
Gamaliel is a doctor : Gamaliel ni daktari
Lulu is a designer : Lulu ni mbunifu.
Goats are in the house : Mbuzi wako kwenye nyumba
4,Verb tells us about a possession : Kitenzi hutuambia kuhusu umiliki wa kitu.
Mfano
I have a good memory ; Mimi nina kumbukumbu nzuri
She has yellow skirt : yeye (she) ana sketi ya njano
(c) Kinds Of Verbs :Aina za Vitenzi
There are basically two main groups of verb
Kuna aina kuu mbili ya vitenzi ,kama ifuataavyo:
- Main Verb : Kitenzi Kikuu
- Auxilliary Verb :Kitenzi Kisaidizi
Mpenzi msomaji katika kipind kinachofuata tutajifunza zaidi kuhusu Main Verb na kujua zinatumikaje katika mazungumzo yetu ya kila siku .
TODAY`S VOCABULARIES : MISAMIATI YA LEO
- boast - majivuno
- boastful - enye majivuno
- bog - ziwa la matope
- bogged down - kukwama,kushindwa kuendesha
- bold - shujaa,jasiri
- boistreous - enye fujo,enye jeuri
- boldness - ushujaa
- bondage - utumwa,kifungonibonfire - moto mkubwa uwashwao kwa sherehe ya jambo fulani
- bonus- - malipo ya ziada baada ya kazi
Ili uweze kufikia lengo lako la kujua kuongea Lugha ya kiingereza ni lazima ujue misamiati mingi,anza sasa kujifunza misamiati kila siku utashangazwa sana na matokeo yake,utakuwa mtaalamu wa lugha,endelea kujumuika nami katika mtandao wa Learn English Language ili kujifunza zaidi kama hujajiunga nasi jiunge sasa kujifunza Lugha ya Kimataifa.
Soma : Powerful word You Can Use to Get Anything
Your Tutor
Jenicia John
Email : jeniciaj55@gmail.com