INTRODUCTION -UTANGULIZI.
Ndugu msomaji karibu sana katika somo hili la leo ambapo ni muhimu sana kabla ya kujifunza sarufi (grammar),kujua lugha ni nini?,ni vitu gani vinaunda lugha?,kwa nini tunapaswa kujifunza lugha na kwa namna gani tunaweza kujifunza lugha.Ulimwenguni pote kuna lugha nyingi sana na kiingereza ni moja wapo,ambayo inajulikana kama lugha ya kimataifa.Hii ni kwa sababu mataifa mengi duniani kiingereza kinatumika katika shughuri mbalimbali,kwa mfano kazini,shuleni na hata kwenye biashara zetu.
Inakuwa njia rahisi sana kujifunza kiingereza kwa kutumia lugha yetu ya taifa (KISWAHILI).Karibu tujifunze pamoja.
Lugha ni nini?- What is Language?
Lugha ni mfumo wa sauti wa sauti zinazotumiwa na watu wa jamii fulani katika mawasiliano.
Language is the system of communication used by people of particular society.
Kwa nini tunajifunza Lugha? - Why we learn language?
Tunajifunza lugha ili itumike katika mawasiliano katika maisha yetu ya kila siku.
We learn language as means of communication in our daily life.
MUUNDO WA LUGHA.
Lugha imeeundwa kwa kwa herufu 26 tu,na herufi hizi zimegawanyika katika makundu mawili:
1.) konsonants/herufi bubu - Consonants
Kuna consonants 21 zinazotumika katika lugha ya kiingerza,na ziko katika herufi kubwa na ndogo kama ifuatavyo:
Bb,Cc,Dd,Ff,Gg,Hh,Jj, Kk,Ll,Mm,Nn,Pp,Qq,Rr,Ss,Tt,Vv,Ww,Xx,Yy,Zz.
2.)Irabu/Vokali - Vowel
Kuna herufi tano tu zinazojulikana kama Irabu..Aa,Ee,Ii,Oo,Uu.
Katika kujifunza lugha ili uweze kupata neno ni lazima pawepo na muunganiko wa konsonantis na irabu ili kupata neno kamili,konsonanti husumama kama baba na irabu husimama kama mtoto.
- Word is the proper combination of letters
Neno NATION limeunndwa kwa consonants na vowel..
- Sentence is the group of words or word which has complete meaning.
- Grammar is the scientific learning of language
Sarufi hutusaidia kuelewa namna lugha inavyoongewa na kuandikwa kwa usahihi na ufanisi zaidi.
Grammar helps us to understand how language is spoken and written in correctly and effectively way.
Hivyo basi Sarufi/grammar inahusika moja kwa moja. katika utungaji wa maneno katika lugha na mgawanyiko wa maneno,sentensi na matumizi yake katika maisha yetu ya kila siku.Kwa leo tuishie hapa usikose somo linalofuata amapo tutajifunza aina za maneno zinazotumika katika lugha ya kiingereza,endelea kuweka jitihada katika kujifunza.
Your Tutor
Jenicia John
Email : jeniciaj55@gmail.com
0 comments:
Post a Comment