Je Unavijua Viwakilishi Milikishi Vinavyotumika Katika Lugha Ya Kiingereza?



Karibu katika somo la leo ambapo tunaendelea kuweka juhudi katika kujifunza lugha ya kimataifa.Leo tutaendelea kujifunza sarufi ya lugha (Grammar),tutajifunza viwakilishi milikishi (Possessive Pronouns)
Karibu tujifunze pamoja.

Possessive Pronouns : Viwakilishi Milikishi
Hivi ni viwakilishi ambavyo vinaonesha umiliki wa kitu au vitu wa mtu yeyote au kitu chochote.Mfano wa maneno yanayoonesha umilikishi ni changu,chake.chao,chetu,vyetu n.k

Yafuatayo ni maneno yanayoonesha viwakilishi milikishi katika lugha ya kiingereza.

1. My / Mine : -angu
    Hiki ni kiwakilishi milikishi cha wewe mwenyewe

Mfano/Example
This is my book : Hiki kitabu ni changu
It  is mine : Ni changu
It is belongs to me :Ninakimiliki mimi

2. Your / Yours : -ako
  Hiki ni kiwakilishi milikishi cha nafsi ya pili,kinaweza wakilisha mtu mmoja au wengi,anaweza kuwa mwanamke au mwanaume au wote kwa pamoja.

Mfano /Example
That is your car : Ile ni gari yako
It is yours : Ni yako

3. Our /Ours : -etu
Hiki ni kiwakilishi milikishi cha wingi,kiwakilishi hiki kinaweza kuwakilisha kundi la wuatu wengi,wanaweza kuwa wanawake au wanaume au wote kwa pamoja.

Mfano / Example
This is our village : Hiki ni kijiji chetu
It is ours : Ni chetu

4. His : -ake
Kiwakilishi hiki huwakilisha umilikishi wa mwanaume tu.

Mfano /Example
This is John's shirt : Hili ni shati la John
This is his shirt : Hili ni shati lake
It is his : Ni lake

5. Her /Hers :-ake
Hiki ni kiwakilishi milikishi kinachowakilisha umilikishi wa mwanamke tu.

Mfano :Example
That is Mariana's house : Ile ni nyumba ya Mariana
That is her house : Ile ni nyumba yake
It is hers : Ni yake

6. Their /Theirs : -ao
Hiki ni kiwakilishi milikishi cha wingi,wanaweza kuwa wanaume kwa wanawake au wote kwa pamoja.

Mfano ?Example
That is their school. : Ile ni shule yao
It is theirs :Ni ya kwao.


Msomaji wa LEARN ENGLISH LANGUAGE hivyo ndio viwakilishi milikishi vinavyotumika katika lugha ya kiingereza.Tuendeelee kuwa pamoja katika masomo yanayofuata ili kujifunza zaidi.Kama hujajiunga na mtandao huu jiunge sasa kujifunza zaidi .Karibu tujifunze pamoja.

Your Tuto
Jenicia John
http://tlearningenglish.blogspot.com




   




Msingi Wa Tano Wa Kujifunza Kuongea Lugha Ya Kiingereza



Ni siku nyingine tena msomaji wa mtandao wa Learn English Language karibu katika somo la leo ambapo tunaendelea kujifunza msingi wa tano wa kujifunza kuongea lugha ya kiingereza.Leo tutajifunza matumizi ya maneno ambayo hutumika sana katika mazungumzo katika maisha yetu ya kila siku.Maneno hayo ni "Trying +To"

 Trying :Haya ni maneno ambayo mtu hutumia kumfahamisha mtu mwingine kwamba anajaribu kwa namna yoyote ile kukamilisha jambo fulani kwa bidii sana.Kwa kuongeza kitenzi "to" ni kuonesha nini hasa ambacho anajaribu kufanya.

Soma:Mbinu za kujifunza lugha ya kiingereza

Pronoun + Trying : These are grammatical words whichi a person use to inform someone else what he/she attempting to accomplish something.By adding the verb "to" is to point out what exactrly you are attempting to do.

Mfano/Example
I am trying to do an exercise everyday
Najaribu kufanya mazoezi kila siku.

 John is trying to find any job to do
 John anajaribu kutafuta kazi yoyote ya kufanya

Children are trying to learn things by themselves
Watoto wanajaribu kujifunza vitu wao wenyewe

I am trying to explain myself to the teacher but she doesnt want to understand me.
Najaribu kujieleza kwa mwalimu lakini hanielewi.

He is trying to work hard.
yeye anajaribu kufanya kazi kwa bidii.

Msomaji  penye nia pana njia endelea kuwa nami ili tuendelee kujifinza,na kama hujajiunga jiunge sasa na mtandao huu ili kujifunza zaidi.Karibu tujifunze pamoja.

Your Tutor
Jenicia John
http://tlearningenglish.blogspot.com



HIVI NDIO VIWAKILISHI VYA NAFSI KATIKA LUGHA YA KIINGEREZA



 Ni siku nyingine tena msomaji wa LEARN ENGLISH LANGUAGE napenda kukukaribisha katika somo la leo ambapo tutajifunza maana ya viwakilishi (pronouns) na viwakilishi vya nafsi (Personal Pronoun) vinavyotumika katika lugha ya kiingereza.Karibu tujifunze pamoja.

PRONOUN : KIWAKILISHI
Pronoun ni neno linalosimama badala ya jina/nomino.
Hii inamaanisha neno hilo linawakilisha jina,viwakilishi vinaweza kusimama badala ya jina la mtu,sehemu,vitu hata wazo.Matumizi ya viwakilishi hayaluhusu majina kuandikwa tena katika sentensi kwa sababu tayari kiwakilishi kimesha wakilisha jina.

Pronoun is a word that stand instead of noun.
This means that pronoun represents nouns.A pronoun can represent a name of  person,place,things or an idea.The use of pronoun does not allow to rename the noun which is represented or replaced in the sentence.

PERSONAL PRONOUNS : VIWAKILISHI VYA NAFSI
Personal Pronouns ni viwakilishi vinavyowakilisha nafsi za watu.Viwakilishi hivi vipo katoka mifumo tofauti kulingana na uwepo wa watu,idadi na jinsia.
Kuna nafsi ya kwanza umoja na wingi ( "I : mimi "and "WE : sisi")
kuna nafsi ya pili umoja na wingi ("you : wewe")
kuna nafsi ya tatu umoja na wingi ("she,he,it" and "They")

Katika lugha ya kiingereza person pronouns zimegawanyika katika makundi saba ambayo ni I,WE,YOU,SHE,HE,IT and THEY.

1. I : MIMI
    Hiki ni kiwakilishi cha nafsi ya kwanza umoja cha jina binafsi.Kiwakilishi hiki hutumika pale mtu         unapojizungumzia wewe mwenywe.Hii ndio sababu inaitwa nafsi ya kwanza umoja.

Mfano /Example
Mimi huwa naenda mjini kila siku
I go to town everyday

2. WE : SISI
    Kiwakilishi hiki ni cha nafsi ya kwanza wingi.Hutumika pale mtu anapozungumzia jambo na yeye anakuwa  mmoja wa wahusika wote.Husimamia majina ya watu wengi,wanaweza kuwa wanawake au wnaume au wote kwa pamoja.
  
    Mfano /Example
     Mimi,John na Neema tunaenda kanisani
     I,John and Neema are going to the church
     We are going to the church.
     Sisi tunaenda kanisani.
    

3. YOU :WEWE /NINYI
     Kiwakilishi hiki husimama badala ya jina moja au mengi,huwakilisha nafsi ya pili umoja na wingi,
     na hutumika kwa jinsia zote.Pia hutumika pale mtu unapomzungumzia mtu mwingine ndio maana
     inaitwa nafsi ya pili.
     
       Mfano /Example
        Wewe lazima ufanye kazi kwa bidii ili ufanikiwe
         You must work hard in order to succeed  

4. THEY : WALE /WAO.
    Kiwakilishi hiki husimamia majina ya watu wengi kwa pamoja wanaweza kuwa wanaume au
    wanawake au wote kwa pamoja.
   
    Mfano / Example
     Jenny na John wanasoma vitabu
     Jenny na John are reading books
     They are reading books

5. HE : YEYE
    Kiwakilishi hiki husimamia jina la wanaume tu.Badala ya kutumia jina la mwanaume yule kiwakilishi
    chake hutumika kiwakiliska jina.
    Mfano / Example
    John ni baba yangu , John huwa ni daktari
    John is my father,John is a doctor.
    He is my father,he is a doctor

6. SHE: YEYE
    Hiki ni kiwakilishi cha nafsi ya tatu umoja,huwakilisha jina la mwanamke tu.Ni nafsi ya tatu umoja
    kwa sababu tunamzungmzia mtu yule na yuko peke yake na jinsia ya kike.
   
Mfano / Example
Mariana ni mwalimu mzuri sana wa saikorojia.
Mariana is a good teacher of psychology.
She is a good teacher of psychology.

7. IT : Ni kiwakilishi kinasimamia majina ya vitu vyote isipokuwa majina ya watu.Lakini pia
          mtoto  mchanga hutumia kiwakilishi hiki.
         
          Mfano /Example
           Ile ni gari yangu,ninaimiliki mimi.
           That is my car,it is belongs to me.
            
          Gari imeibiwa         
          A car has stolen
          It has stolen


Msomaji wa mtandao wa LEARN ENGLISH LANGUAGE tutaendelea kujifanza viwakilishi vingine vinavyotumika katika lugha ya kiingereza.Endelea kuwa nasi  na kama hujajiunga na mtandao huu jiunge sasa ili kuweza kujifunza zaidi lugha ya kimataifa.

Your Tutor
Jenicia John
http://tlearningenglish.blogspot.com



 
     





MSINGI WA NNE WA KUJUA KUONGEA KIINGEREZA




 Karibu katika somo la leo tunaendelea kujifunza misingi mbalimbali ya kujua kuongea lugha ya kiingereza.Siku ya leo tutajifunza matumizi ya neno "going to".Namna linavyotumika katika mazungumzo yetu ya kila siku.Karibu tujifunze pamoja.

"Going to" ni neno ambalo hutumika kumwelezea mtu ulichopanga kufanya wewe au mtu mwingine kwa sasa au unachotarajia kufanya kwa baadae.

"Going to" is the grammatical word which used when you are telling someone what you are planning to do at the moment or in the near future.

Mfano : Example
I am going to work.
Naenda kufanya kazi

Neema is giong to prepare dinner
Neema ataandaa chakula cha usiku

I am going to stop drinking alcohol
Nitaacha kunywa pombe

Sherry is going to help her friend to find job
Sherry atamsaidia rafiki yake kutafuta kazi

Our teacher  is going to teach us Maths
Mwalimu wetu ataatufundisha Maths

I am going to stop smoking
Nitaacha kuvuta sigara

She is going to read all those books
Yeye atasoma vile vitabu vyote.



 EXERCISE : ZOEZI



Msomaji wa LEARN ENGLISH LANGUAGE tutaendelea kujifunza maneno mengi zaidi yanayotumika katika maisha yetu ya kila siku,hii ndio misingi ya kujua kujifunza kuongea lugha ya kiingereza.

Your Tutor
Jenicia John
http://tlearningenglish.blogspots.com