Je Unavijua Viwakilishi Milikishi Vinavyotumika Katika Lugha Ya Kiingereza?



Karibu katika somo la leo ambapo tunaendelea kuweka juhudi katika kujifunza lugha ya kimataifa.Leo tutaendelea kujifunza sarufi ya lugha (Grammar),tutajifunza viwakilishi milikishi (Possessive Pronouns)
Karibu tujifunze pamoja.

Possessive Pronouns : Viwakilishi Milikishi
Hivi ni viwakilishi ambavyo vinaonesha umiliki wa kitu au vitu wa mtu yeyote au kitu chochote.Mfano wa maneno yanayoonesha umilikishi ni changu,chake.chao,chetu,vyetu n.k

Yafuatayo ni maneno yanayoonesha viwakilishi milikishi katika lugha ya kiingereza.

1. My / Mine : -angu
    Hiki ni kiwakilishi milikishi cha wewe mwenyewe

Mfano/Example
This is my book : Hiki kitabu ni changu
It  is mine : Ni changu
It is belongs to me :Ninakimiliki mimi

2. Your / Yours : -ako
  Hiki ni kiwakilishi milikishi cha nafsi ya pili,kinaweza wakilisha mtu mmoja au wengi,anaweza kuwa mwanamke au mwanaume au wote kwa pamoja.

Mfano /Example
That is your car : Ile ni gari yako
It is yours : Ni yako

3. Our /Ours : -etu
Hiki ni kiwakilishi milikishi cha wingi,kiwakilishi hiki kinaweza kuwakilisha kundi la wuatu wengi,wanaweza kuwa wanawake au wanaume au wote kwa pamoja.

Mfano / Example
This is our village : Hiki ni kijiji chetu
It is ours : Ni chetu

4. His : -ake
Kiwakilishi hiki huwakilisha umilikishi wa mwanaume tu.

Mfano /Example
This is John's shirt : Hili ni shati la John
This is his shirt : Hili ni shati lake
It is his : Ni lake

5. Her /Hers :-ake
Hiki ni kiwakilishi milikishi kinachowakilisha umilikishi wa mwanamke tu.

Mfano :Example
That is Mariana's house : Ile ni nyumba ya Mariana
That is her house : Ile ni nyumba yake
It is hers : Ni yake

6. Their /Theirs : -ao
Hiki ni kiwakilishi milikishi cha wingi,wanaweza kuwa wanaume kwa wanawake au wote kwa pamoja.

Mfano ?Example
That is their school. : Ile ni shule yao
It is theirs :Ni ya kwao.


Msomaji wa LEARN ENGLISH LANGUAGE hivyo ndio viwakilishi milikishi vinavyotumika katika lugha ya kiingereza.Tuendeelee kuwa pamoja katika masomo yanayofuata ili kujifunza zaidi.Kama hujajiunga na mtandao huu jiunge sasa kujifunza zaidi .Karibu tujifunze pamoja.

Your Tuto
Jenicia John
http://tlearningenglish.blogspot.com




   




4 comments:

  1. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  2. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  3. You are very genius teacher
    Thanks
    Continue don't hesitate to do so
    We're together
    Thanks so much

    ReplyDelete