HUU NDIO MSINGI WA TATU WA KUJUA KUONGEA LUGHA YA KIINGEREZA



Habari msomaji wa LEARN ENGLISH LANGUAGE ni siku nyingine tena napenda kukukaribisha katika somo la leo ambapo tutajifunza msingi wa 3 wa kujua kuongea kiingereza,Msingi huu ni maneno ya kawaida kabisa ambayo yanatumika katika maisha yetu ya kila siku,leo tutajifinza matumizi ya neno "good at"

"GOOD AT"
Hili ni neno ambalo hutumika kuelezea uwezo wa mtu alionao katika kufanya jambo fulani kwa umakini wa hali ya juu kwa sababu yeye ni mtaalamu katika jambo lile.Angalia sentensi zifuatazo:

Mfano:
1. I am good at cooking
    Mimi ni mzuri sana katika mapishi
    Hii inamaanisha mimi nina uwezo mzuri sana katika kupika

2. Neema is good at dancing music
    Neema ni mzuri sana katika kucheza mziki

3.Children are good at playing football
   watoto ni wazuri sana katika kucheza mpira.

4. Asha is good at writting novel
    Asha ni mzuri sana katika uandishi wa riwaya

5. We are good at swimming
     Sisi ni wazuri sana katika kuogerea

6. They are good at conducting research
     Wao ni wazuri sana katika kufanya utafiti

7.John and Jack are good at driving a car.  
   John na Jack ni wazuri sana katika kuendesha gari.

8. Jenny is good at English Language and French
    Jenny ni mzuri sana katika lugha ya Kiingereza na Kifaransa

Sentensi hizi zote zinaonyesha watu hawa wanauwezo wa kufanya jambo fulani vizuri  kwa ufanisi na usahihi zaidi.Msomaji wa Learn English Language tutaendelea kujifunza maneno mengi zaidi ambayo yanatumika katika maisha yetu ya kila siku,maneno haya yanaweza kuwa mwongozo na msingi wa kujua kuongea lugha ya Kiingereza.Kama hujajiunga na muandao huu jiunge sasa tujifunze pamoja.

Your Tutor
Jenicia John
http:/tlearningenglish.blogspot.com

0 comments:

Post a Comment