MSINGI WA PILI WA KUJUA KUONGEA KIINGEREZA



Habari msomaji wa LEARN ENGLISH LANGUAGE karibu katika somo la leo ambapo tutajifunza msingi wa pili wa kujua kongea lugha ya kiingereza.Nauita ni msingi kwa sababu ni maneno ambayo yanatumika katika maisha yetu ya kila siku.Leo tutajifunza matumizi ya neno "I AM IN" na "I AM AT"

I AM IN - NIKO KWENYE AU NIKO NDANI YA...
Maneno haya hutumika kuelezea uko ndani ya kitu fulani au unaelezea jambo ambalo nafanya.
Angalia sentensi zifuatazo kujifunza zaidi;

1: I am in the school - Niko kwenye shule au niko shuleni
    Hii inamaanisha ndani ya shule

2: I am in the house - Niko kwenye nyumba
    Hii inamaanisha nimeingia ndani ya nyumba

3: I am in the kitchen - Niko jikoni
    Hii inamaanisha nimeingia ndani ya chumba cha kupikia/jikoni

4: I am in the box - Niko kwenye boksi
    Hii inamaanisha nimeingia ndani ya boksi

5: I am in the car - Niko kwenye gari
     Hii inamaanisha niko ndani ya gari




 "I am in the box" child said
  "Niko kwenye boks" Mtoto alisema







 

 One of them answered her phone said"i am in the car"


 Mmoja wao alijibu simu yake akasema "niko kwenye gari"




I AM AT - NIKO SEHEMU
Neno hili hutumika kumwelezea mtu sehemu ulipo  kwa wakati huo.
Mfano:
1. I am at the grocery - Niko kwenye mgahawa/
    Hii inamaanisha niko sehemu / maeneo ya mgahawa

2. I am at the airpot - Niko uwanja wa ndege
    Hii inamaanisha niko sehemu / maeneo ya uwanja wa ndege

3. I am at the Whitehouse - Niko Ikulu
    Hii inamaanisha niko sehemu au maeneo ya Ikulu
                       



 I am at beach
 Niko ufukweni mwa bahari (hii ni sehumu au eneo)







NOTE: Kuna wakati matumizi ya maneno haya yanaweza kukuchanganya,hebu angalia kwa makini sentensi zifuatazo zinafanana lakini zina maana tofauti kabisa;

1. I am in the supermarket.
2. I am at the supermarket.

Sentensi ya kwanza inamaanisha sehemu / eneo la supermarket.
Sentensi ya Pili inamaanisha niko ndani ya jengo la supermarket.

 3. I am at the police station.
 4. I am in the police station.

Sentensi ya kwanza namuelezea mtu kuwa niko sehemu /eneo la kituo cha polisi
Sentensi ya Pili namuelezea mtu kuwa niko ndani ya jengo la kituo cha polisi.

Somo letu la leo limeishia hapo,tutaendelea kujifunza zaidi misingi ya namna ya kujua kuongea kiingereza,endelea kufuatilia masomo yanayofuata,kama hujajiunga jiunge sasa na mtandao wa LEARN ENGLISH LANGUAGE ili kujifunza zaidi lugha ya kimataifa,Karibu tujifunze pamoja.

Your Tutor
Jenicia John
http://tlearningenglish.blogspots.com

    

   

0 comments:

Post a Comment