Karibu katika somo la leo ambapo tutajifunza Countable nouns na Uncountable nouns.Somo la leo litatusaidia kuelewa majina ya vitu vinavyohesabika na visivyohesabika,haya yanaweza kuwa majina ya watu au majina ya vitu.Karibu tujifunze pamoja.
COUNTABLE NOUNS - MAJINA YANAYOHESABIKA
Countable nouns ni majina ya vitu ambavyo vinaweza kuhesabika.Majina haya yanaweza kuwekwa katika hali ya umoja na wingi.
Countable nouns are names of things which can be counted.These names can be categorized ino singular and plural.
Mfano:Example
- cow - ng'ombe
- tree - mti
- house - nyumba
- woman - mwanamke
- man - mwanaume
- book - kitabu
- church - kanisa
- student - mwanafunzi
UNCOUNTABLE NOUNS : MAJINA YASIYOHESABIKA
Uncountable nouns ni majina yavitu ambavyo havihesabiki ,wala hayawezi kuwa katika umoja na wingi.
Uncountable nouns are names of things which can not be counted or divided into singular and plural.
Mfano : Example
- milk - maziwa
- water - maji
- rice - mchele
- honey - asali
- butter - siagi
- flour - unga
- sand - mchanga
Mfano:
- three spoon of sugar - vijiko vitatu vya sukari
- ten bottle of water - chupa kumi za maji
- two bags of rice - mifuko miwili ya mchele
TODAY'S VOCABULARIES : MISAMIATI YA LEO
Vocabulary/msamiati Pronounciation/matamshi Meaning/maana
accident -aksident -tukio la ajari
acclaim -akleim -pokea kwa shangwe
acclamation -aklemeshen -vegeregere,vifijo
accord -akod - mapatano
accompany -akampany - fuatana na..,ongozana
accomplish - akomplish - timiza,tekeleza
Mwisho wa somo letu la leo,kama hujajinga na mtandao huu wa LEARN ENGLISH LANGUAGE jiunge sasa ili tuendelee kujifunza lugha ya kimataifa.kama umejiunga tuatumiwa email ya mafunzo kila siku kwr
enye email yako.Karibu tujifunze pamoja.
Your Tuto
Jenicia John
http://tlearningenglish.blogspot.com
Thank you my tutor J, I have understood it clearly.
ReplyDelete